Habari za Simba SC
Habari za michezo

BAADA YA KUONA ANAZIONEA SANA TIMU NDOGO NDOGO…MBRAZILI SIMBA KATAKA HAWA SASA..

admin September 7, 2023 10:58 am

Kocha wa Simba Robertinho amesema anahitaji mechi moja ya kimataifa nje ya Tanzania kutokana na kuanza na mchezo wa Ligi ya Mabingwa ugenini dhidi ya Power Dynamos ya Zambia mchezo utakaopigwa Septemba 16.

Alisema kwa upande wa maandalizi ya ndani alimaliza na keshaongea na viongozi wamtafutie mechi ya kimataifa ambayo watacheza ugenini ili kujiweka tayari na mchezo wa kimataifa.

“Mchezo unaofuata tunacheza nje ya Dar es Salaam, hivyo na mimi nahitaji mechi moja ya kirafiki ya kimataifa ambayo itachezwa nje ya Tanzania,” alisema.

Mratibu wa Simba, Abbas Ally alisema kuwa kuhusiana na hilo, ni kweli walikuwa na mpango wa kwenda Kenya kwa ajili ya mechi mbili za kirafiki na walipata mwaliko wa kucheza dhidi ya Police na Gor Mahia, lakini hawatafanya hivyo.

“Tulipata mechi mbili za kirafiki, lakini Chama cha Soka cha Kenya kimetuomba kucheza mechi hizo bila kuruhusu mashabiki kitu ambacho siyo rahisi kutokana na ukubwa wa timu yetu ambayo ina mashabiki wengi kila upande, hivyo tunahofia watajitokeza kwa wingi na sisi tukaonekana tumewadharau,” alisema.

KWA YANGA NZIMA…HUYU HAPA NDIYE STAA ANAYEMTIA ‘TUMBO JOTO’ KOCHA WA EL MERREIKH… ZINGATIA ALAMA HIZI ZA USHINDI KWENYE JACKPOT LAB NDANI YA MERIDIANBET…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply