Taifa Stars
Habari za michezo

BAADA YA TANZANIA KUFUZU AFCON MWAKANI….MASTAA WOTE KULAMBA BINGO HILI…

admin September 8, 2023 4:52 pm

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ametekeleza ahadi ya Shilingi milioni 500 aliyotoa kwa Timu ya Taifa Stars ikifuzu kucheza Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2023 nchini Ivory Coast.

Akizungumza na wachezaji na viongozi wa timu hiyo Septemba 7, 2023 nchini Algeria, Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Saidi Yakubu ambaye aliongoza msafara wa timu hiyo, amewapongeza wachezaji na benchi la ufundi kwa kazi kubwa waliyofanya.

“Kwa niaba ya Serikali, Mhe. Rais, Mhe. Waziri pamoja na wadau wote, tumekuja hapa kuongeza hamasa. Kubwa mtakumbuka wakati wa kujiandaa na mechi ya Uganda kule nyumbani Mhe. Rais alitoa ahadi ya kutoa Shilingi milioni 500, timu ikifuzu.

“Nafurahi kuwaambia kwamba hizo fedha sio tu kwamba zitatolewa, zimekwisha letwa Wizarani kwa ajili yenu,” alisema Yakubu.

MCHAMBUZI: AHMED ALLY ANAIDHARAULISHA SIMBA…. MWAKA MMOJA TOKA ASEPE YANGA….YACOUBA AANIKA SIRI KIBAO YA AZIZ KI…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply