Home Habari za michezo KUHUSU KUCHEZA NA TIMU DHAIFU….KIGOGO SIMBA AFICHUA MIPANGO YAO ILIVYOKUWA…

KUHUSU KUCHEZA NA TIMU DHAIFU….KIGOGO SIMBA AFICHUA MIPANGO YAO ILIVYOKUWA…

Habari za Simba

Simba imecheza michezo miwili ya kirafiki dhidi ya Kipanga ambapo walishinda mabao 5-1, kisha juzi Jumanne wakacheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Cosmopolitan na kuibuka na ushindi wa mabao 3-0.

Sasa wadau wa soka walilalamika kuwa inakuaje Simba anacheza mechi za kirafiki na timu ndogo na zisizo na ushindani hali ya kuwa ana mchezo mgumu na wa ushindani dhdi ya Power Dynamos mchezo wa kuwania kufuzu hatua ya Makundi Ligi ya Mabingwa Afrika.

Sasa Msemaji wa Simba amefafanua kuhusiana na maneno hayo;

“Katika kujenga kikosi au pre-season sio lazima kucheza mechi ngumu. Tumecheza mechi Mbili (2) dhidi ya Kipanga na Cosmopolitan”

“Faida ya kucheza mechi nyepesi ni kuwapa fursa kucheza hata wachezaji ambao hawapati nafasi kikosini, kwenye mechi ngumu wachezaji hucheza kwa presha uwanjani wakiogopa kukosea”

SOMA NA HII  KUELEKEA MAKUNDI CAF...SIMBA NA WABABE WA YANGA WAWEKWA KAPU MOJA....ISHU ITAKUWA HIVI...