Tetesi za Usajili Simba
Habari za michezo

SIMBA SC WATAJWA BUNGENI TENA….ISHU NZIMA IKO HIVI….

admin September 8, 2023 7:41 pm

Waziri Mkuu, Mh. Kassim Majaliwa ameipongeza Simba kwa  kuwa miongoni mwa klabu nane zitakazoshiriki michuano mipya ya African Football League (AFL) ambayo itaanza Oktoba 20.

Mh. Majaliwa ameyasema hayo Bungeni jijini Dodoma leo ambapo Simba inaitangaza nchi kimataifa na hilo ni jambo la kupongezwa.

“Mh. Spika nichukue nafasi hii kuipongeza klabu ya Simba kwakuwa moja ya timu nane bora barani Afrika ambayo itashiriki michuano ya African Football League.

“Hii ni heshima kubwa kwa Taifa ambayo Simba imeileta. Ufunguzi wa michuano hii itafanyika jijini Dar es Salaam Oktoba, 20 hivyo nawaomba mashabiki mjitokeze kwa wingi siku hiyo,” amesema Waziri Mkuu Majaliwa.

Katika mchezo huo wa ufunguzi utakaopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa, Simba itacheza na miamba ya Afrika, Al Ahly kutoka Misri.

SIRI YA MAZOEZI MAGUMU YANGA HII HAPA….GAMONDI AOMBA MECHI YA HARAKA…. KWA YANGA HII, WATAKE WASITAKE WATAPIGWA TU…. WACHEZAJI WAMPANDISHA MZUKA GAMONDI

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply