Habari za michezo
KRAMO TIA MAJI TIA MAJI MAPYA YAIBUKA SIMBA
Staff Desk
September 9, 2023
3:52 pm
Nyota wa Simba SC Aubin Kramo amepata majeraha ya goti kwenye mchezo wa kirafiki hii leo dhidi ya Ngome FC mchezo ambao Simba waliibuka na ushindi wa mabao 6-0
Kramo alitolewa dakika ya 42 ya mchezo akimpisha Jean Baleke akiwa ameshafunga bao moja.
Mchezaji huyo ndio kwanza alikuwa anarudi kutoka katika majeraha ambayo yamemuweka nje tangu kuanza kwa msimu 2023/24.
Ni wakati Mgumu kwake, Get well soon Aubin!
Leave a Reply
You must be logged in to post a comment.