Afisa Habari wa Yanga SC Ally Kamwe
Habari za michezo

KUHUSU ISHU YA MASHABIKI KUSHINDWA KUANGALIA MECHI RWANDA, UONGOZI WA YANGA WASEMA HAYA

Staff Desk September 12, 2023 10:59 am

Afisa Habari wa Yanga SC, Ally Kamwe amesema, mashabiki wote watakaosafiri na mabasi kwenda Rwanda kwa ajili yua mchezo wao wa Klabu Bingwa dhidi ya Al Merrikh, wataingia uwanjani kushuhudia mtanange huo.

Kamwe ametoa kauli hiyo leo Septemba 12, 2023 kufuatia kuwepo kwa taarifa za chini chini za kwamba huwenda wapinzani wao wakawapa tiketi chache hivyo mashabiki wa Yanga kushindwa kuingia uwanjani.

“Hizi taarifa zimeibuliwa na watu wanaopenda kupelekwa mjini na sisi tumesema safari hii hatumpeleki mtu mjini. Yanga inaongozwa na viongozi makini wenye weledi, tumeshafanya mawasiliano na wenzetu kule Shirikisho la Mpira Rwanda na kila kitu kipo sawa, mashabiki wasiwe na hofu,” alisema Kamwe.

GAMONDI : MECHI HII NI NGUMU ILA ITAFAHAMIKA HUKO HUKO NIYONZIMA NA YANGA MPAKA MAKUNDI CAF

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply