Habari za Simba
Habari za michezo

CHAMA:- POWER DYNAMOS WA SIMBA DAY …SIO HAWA…HAWA NI WENGINE…

admin September 14, 2023 6:21 pm

KIUNGO mshambuliaji wa Simba, Mzambia, Clatous Chama amesema wapo  tayari kwa mapambano katika mchezo wao wa hatua ya pili ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Power Dynamos ya Zambia.

Simba imesafiriki kuelekea nchini Zambia kwa ajili ya mchezo huo utakaopigwa katika dimba la Levy Mwanawasa, Ndola Nchini huko dhidi ya wenyeji wao hao.

 Chama alisema wameshacheza na Power Dynamos mara mbili katika tamasha la Simba Day na wamezidi kuwa imara.

Alisema wanaenda kukutana na timu ambayo iliyokuwa imara na wanatakiwa kuwsheshimu wapinzani wao kwa sababu ya ubora walikuwa nao kwa sasa.

“Power Dynamos tuliyocheza nao katika Simba Day sio tuyakayo kwenda kucheza kwenye mashindano hayo, watakuja kivingine, hata sisi tumejipanga na matarajio yetu makubwa kuvuka hatua iliyopo mbele yetu.

“Tuko tayari kukutana na wapinzani wetu, tutapambana kwa ajili ya timu , kila mmoja anahitaji mafanikio ambayo tunayoyatarajia kuvuka katika kila hatua na kucheza nusu fainali ambayo ni malengo yetu,” alisema Chama.

Aliongeza kuwa hawatawadharau wapinzani wao na kuhakikisha wanapambana kutafuta ushundi katika mchezo huo wa ugenini na kurejea nyumbani kumaliza mchezo.

BAADA YA KUPATA ‘PANCHA’ INGINE….KRAMO NNJE WIKI MBILI…. SASA UNAWEZA KUANGALIA MKEKA WAKO WA MERIDIANBET ‘LIVE’ NDANI YA MAX 99 UKIWA MBAGALA….

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply