Habari za Michezo
Habari za michezo

KUNA NINI SINGIDA….?..KOCHA MPYA ADAIWA KUTIMKA….MASTAA HAWA WATAJWA…

admin September 19, 2023 3:54 pm

Kocha wa Singida Ernst Middendorp ameripotiwa kung’atuka klabuni hapo ikiwa ni chini ya mwezi tu tangu ashike hatamu ya kukinoa kikosi hicho huku aliyekuwa kocha msaidizi Mathias Luke akirejeshwa klabuni hapo kushika hatamu kama kocha wa muda.

Inaelezwa kocha huyo ametofautiana na bosi wa klabu hiyo aliyeripotiwa kuhoji kwanini kocha huyo hakuwapanga baadhi ya wachezaji kwenye mchezo dhidi ya Future FC ambao klabu hiyo ilishinda 1-0 na kuamua kutimka akidai hawezi kuingiliwa majukumu kwa kuwa anaamini anachokifanya.

Hata hivyo Afisa Habari wa Singida Big Stars, Hussein Masanza akijibu kuhusu kung’atuka kwa Mjerumani huko amesema “Kocha Ernst amepata dharura na ameondoka kwa dharura”

Masanza ametoa ufafanuzi huo leo akiwa katika dimba la Uhuru Dar es Salaam ambako kikosi cha Singida Fontaine Gate FC kinaendelea kujifua.

KISA SARE NA WAZAMBIA…BOSI ‘KAZI’ SIMBA AJIAPIZA ‘KUFANYA JAMBO’ MECHI YA DAR… PAMOJA NA ‘KUWAZAGAMUA’ WASUDAN JUZI…MASTAA YANGA WAPEWA ONYO KWA NAMUNGO…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply