Home Habari za michezo BAADA YA KUWAVURUGA MAZIMA RWANDA….YANGA WAIPOTEZEA ‘KIMTINDO’ AL MERRIKH…

BAADA YA KUWAVURUGA MAZIMA RWANDA….YANGA WAIPOTEZEA ‘KIMTINDO’ AL MERRIKH…

Habari za Yanga

Uongozi wa Young Africans umewapotezea kimtindo wapinzani wao AI Merrikh kuelekea kwenye mchezo wao wa Mkondo wa Pili wa Ligi ya Mabingwa Barani Afrika kwa kuamua kuwekeza nguvu kubwa kwenye ligi.

Young Africans chini ya Kocha Mkuu, Miguel Gamondi ina kibarua cha kusaka ushindi dhidi ya Al Merreikh wakiwa na kumbukumbu ushindi wa mabao 0-2 ya ugenini.

Mchezo wao wa marudio ambao utatoa mshindi atakayefuzu hatua ya makundi kwenye Ligi ya Mabingwa Barani Afrika unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Azam Complex.

Leo Jumatano (Septamba 20) Young Africans watacheza na Namungo FC ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Bara ambao unatarajiwa kupigwa uwanjani hapo.

Kwenye mchezo huo, kocha wa Young Africans, Miguel Gamondi huenda akafanya mabadiliko makubwa juu ya kikosi chake kitakachoanza ikiwa ni baada ya kupata taarifa za uwepo wa mashushushu wa wapinzani wao, Al Merrikh ambao wenyewe wanataka kuutumia mchezo huo kama sehemu ya kujiandaa na mchezo wao wa marudiano.

Ofisa Habari wa Young Africans, Ally Kamwe amesema kuwa kwa sasa hawafikirii kuhusu mchezo wao wa kimataifa ambao upo mbele yao.

“Kuhusu mchezo wetu dhidi ya Al Merrikh ambao ni wa kimataifa kwa sasa hatufikirii sana kwa sababu kuna mechi ya ligi ambayo hiyo ni muhimu kwetu kupata ushindi.

Tukimaliza kazi yetu kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Namungo FC hapo mipango itaanza kwa ajili ya mchezo wetu unaofuata, kwanza tupate burudani ya ndani unajua ligi yetu ina ushindani mkubwa pointi tatu ni muhimu kweli,” amesema Kamwe.

SOMA NA HII  AZAM FC WAGOMEA MAKOCHA WABONGO...IBENGE KUMWAGA WINO