Home Habari za michezo SIMBA , YANGA ZAPEWA ‘UCHAWI’ KUBEBA TAJI LIGI YA MABINGWA AFRIKA…

SIMBA , YANGA ZAPEWA ‘UCHAWI’ KUBEBA TAJI LIGI YA MABINGWA AFRIKA…

Habari za Yanga leo

SIMBA na Yanga siyo ishu tena kushinda ugenini katika michuano ya CAF, isipokuwa zimeshauriwa kuweka nguvu katika mataji, ili kuandika historia.

Wachezaji wa zamani wa timu hizo wanaona ni wakati wa kuchukua mataji ya CAF wakitolea mfano wa Yanga ilivyotinga fainali Kombe la Shirikisho Afrikadhidi ya USM Alger msimu uliopita.

Kocha wa zamani wa Simba, Abdallah Kibadeni alisema kuweza kupata matokeo ugenini kwa kujiamini kunatafsiri kuwa hakuna linaloshindikana.

“Mfano Yanga haikuwa bahati yao michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika msimu uliopita, ilifanya vizuri hadi kucheza fainali, hivyo klabu hizo kongwe inawezekana kabisa zikafanikisha taji hilo,” alisema.

Kipa wa zamani wa Yanga, Benjamin Haule aamini kuna kila sababu wa klabu hizo kongwe kuandika rekodi akitoa sababu za usajili dhidi ya timu wanazoshindana nazo kwenye michuano hiyo.

“Simba na Yanga zinasajili mastaa dhidi ya timu wanazoshindana nazo CAF, mfano Stephen Aziz Ki wa Yanga, kwa Simba Moses Phiri. Hao ni baadhi tu, ubora wa mastaa unaweza kuziwezesha kutwaa ubingwa siku za usoni,” alisema.

SOMA NA HII  KARIA: LIGI BONGO HATASIMAMA KISA KOMBE LA DUNIA...KUNA TIMU IKIFUNGWA NATUKANWA MIMI....