Home Habari za michezo ROBERTINHO:- COSTAL UNION WAMETUPA DAWA YA KUTINGA MAKUNDI CAF….

ROBERTINHO:- COSTAL UNION WAMETUPA DAWA YA KUTINGA MAKUNDI CAF….

Habari za Simba

BAADA ya kuvuna pointi tatu dhidi ya Coastal Union, mchezo wa Ligi Kuu Bara, Kocha Mkuu wa Simba, Roberto Oliviera ‘Robertinho’, ameweka wazi mechi hiyo ameitumia kwa ajili ya kuandaa siraha zake kuelekea mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika.

Amesema kwenye mechi hiyo ameangalia mambo mawili makubwa ikiwemo mbinu mpya aliyowapa wachezaji wake na kuwatumia wale wenye uzoefu ili kuzidi kutengeneza uelewano kuelekea mechi hiyo ya Kimataifa dhidi ya Power Dynamos ya Zambia.

Simba inatarajia kushuka dimbani Jumapili ya Oktoba Mosi, mwaka huu Uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi, Dar es Salaam ikiwakaribisha Power Dynamos kwenye mechi ya marudiano ya Ligi ya Mabingwa Afrika na Robertinho ametumia mechi na Coastal Union kuwa maandalizi ya mchezo huo.

Baada ya kukamilika kwa dakika tisini juzi katika Uwanja wa Uhuru, Simba akivuna alama tatu mbele ya wenyeji wao Coastal Union kichapo cha mabao 3-0, kocha Robertinho alisema mechi hiyo ni kipimo kizuri kujiandaa dhidi ya Power Dynamos.

Alisema katika mchezo wao na Coastal Union ametumia wachezaji wenye uzoefu ili kuzidi kutengeneza maelewano baini yao kuelekea mchezo huo wa kutafuta nafasi ya kufuzu kucheza hatua ya makundi ya Ligi ya Afrika.

“Baada ya kucheza mechi yetu ya kwanza, Zambia tulitoka sare ya mabao 2-2, tuliona jinsi walivyocheza na tuliporejea tukafanyia kazi changamoto zetu na kuwaongeza kitu ambacho leo wamekifanya nilivyowaangiza.

“Nimefurahishwa jinsi wachezaji walivyocheza ninaimani tulikuwa na nafasi ya kupata mabao mengi zaidi ya matatu tuliyofunga, tumeutumia mchezo wa leo (juzi) kujiandaa na mechi ya marudiano ya ligi ya Mabingwa dhidi ya Power Dynamos,” alisema Robertinho na aliongeza kuwa;

“ Tulijua Coastal Union watatupa mechi ngumu ambayo itazidi kutuimarisha, ukiangalia kikosi chetu leo (jana) tumewatumia wachezaji wenye uzoefu ambao tunategemea kuwatumia dhidi ya Power Dynamos,” alisema Robertinho.

Kuhusu ushindi wa mabao huo, Kocha huyo alisema walikuwa na nafasi kubwa ya kupata idadi kubwa ya mabao kuanzia sita hadi saba lakini kupata matatu sio mbaya.

SOMA NA HII  SIMBA YAPANIA KUFANYA KWELI KWA MKAPA MBELE YA KAIZER CHIEFS