Habari za michezo

ISHU YA SIMBA NA MANULA IMEFIKA PATAMU SASA

Staff Desk September 23, 2023 11:50 am

Mlinda Mlango wa Klabu ya Soka ya Simba, Aish Salum Manula ameonekana kuimarika zaidi baada ya kuwa nje ya Uwanja kwa Muda Mrefu kutokana na jeraha la lake.

Kipa huyo ameonekana akifanya mazoezi na kikosi cha kwanza cha Kocha Robertinho baada ya madaktari kuthibitisha kuwa yupo fiti na anaweza kurejea Uwanjani muda Wowote kuanzia sasa.

Imeelezwa kuwa, Manula amepona kabisa majeraha yake na kilichobaki ni kurejesha fitness yake ili benchi la ufundi waanze kumtumia kwenye mechi za kimashindano.

Manula amekuwa nje ya uwanja kwa zaidi ya miezi mitano akijiuguza baada ya kufanyiwa upasuaji nchini Afrika Kusini kufuatia majeraha aliyoyapata mwishoni mwa msimu uliopita.

HILI HAPA DONGO LA SHAFFIH DAUKA KWA MASHABIKI WA SIMBA NA TIMU YAO…. HATIMA YA TANZANIA KUANDAA AFCON 2027 KUJULIKANA WIKI IJAYO…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply