Habari za Yanga SC
Habari za michezo

LOMALISA AFUNGUKA KUHUSU RAFU HII ILIYOMTOA MACHOZI

Staff Desk September 25, 2023 8:00 pm

Beki wa kushoto wa Yanga, Joyce Lomalisa amekiri rafu aliyofanyiwa na Hashimu Manyanya wa Namungo katika mchezo wa raundi ya tatu Ligi Kuu uliomalizika kwa ushindi 1-0 katika Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Septemba 20 ilimfanya angue kilio.

Beki huyo akizungumza nasi nakusema kwamba alitokwa na machozi baada ya jaribio la kutaka kuendelea na mchezo huo kushindikana kwa kuwa nia yake ilikuwa ni kuipambani timu.

Lomalisa amesema alitaka kuendelea na mchezo ili aisaidie Yanga ambayo ilikuwa inatafuta ushindi na ulipopatikana ulikuwa umemfuta machozi, huku akionyesha kutofurahishwa na alivyochezewa.

“Sikufikiria kama angefanya kitu kama kile, ndio maana nilienda kwa lengo la kuuchukua mpira pekee, lakini baadaye nikaona amekuja vibaya na aliniumiza sana,” amesema Lomalisa ambaye alitolewa akichechemea baada ya kipindi cha pili kuanza na nafasi yake kuchukuliwa na Nickson Kibabage.

“Nilitaka kuendelea na mchezo ingawa nilikuwa nasikia maumivu, lakini baadaye nikashindwa kabisa na kuomba kutoka. Ni kweli nililia unajua mpaka natoka tulikuwa hatujapata bao na mechi ilikuwa ngumu. Niliumia kuona nashindwa kuendelea kuitumikia timu yangu ikiwa inatafuta ushindi muhimu.”

MASTAA HAWA WA YANGA WAMCHANGANYA KOCHA WA AL MAREIKH MITEGO MIWILI YANGA HII HAPA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply