Home Habari za michezo UNAAMBIWA GAMONDI HATAKI UTANI AHAMISHIA MAJESHI UPANDE HUU

UNAAMBIWA GAMONDI HATAKI UTANI AHAMISHIA MAJESHI UPANDE HUU

BAADA ya kufanikiwa kwenye safu ya ushambuliaji, Kocha Mkuu wa Yanga, Miguel Angel Gamondi amehamisha silaha zake kwa safu ya ulinzi kuwa makini na kutofanya makosa kwenye mechi ya marudiano ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya El Merrikh ya Sudan.

Amesema hawajaruhusu bao kwenye mechi za ushundani lakini anahitaji mabeki kuongeza umakini zaidi kuelekea mchezo wa Jumamosi akitarajia El Merrikh watakuwa kivingine zaidi ili kulipa kisasi.

Safu ya ulinzi ya Yanga inaongozwa na nahodha Bakari Mwamnyeto, Ibrahim Bacca, Attohoula Yao, Dickson Job na Gift Freddy anbaye hajapata muda wa kucheza mechi ya kimataifa kutokana na changamoto za ushundani wa namba ndani ya kikosi cha timu hiyo.

Yanga watakuwa wenyeji kuwakabili wapinzani wao El Merrikh, mchezo wa marudiano utakaochezwa kesho , uwanja wa Azam, Chamazi Dar-es-Salaam saa 1:00 usiku wakati mechi ya kwanza ilikuwa 2-0.

Katika mazoezi ya juzi na jana uwanja wa Avic Town , Kigamboni ,Gamondi alikuwa makini zaidi kuwapa maelekezo mabeki kupunguza makosa yanayotokanayo na mipira ya kutenga.

Gamond alisema licha ya kutoruhusu bao lakini bado kuna makosa ya mipira ya kutenga wanatakiwa kufanyia kazi kwa sababu ya ubora wa Al Merrikh.

Alisema siyo vizuri kwa walinzi kuwa na makosa katika eneo la hatari, ni bora makosa madogo yafanyike katika maeneo mengine lakini sio katika hatari kwa kuwa yanaweza kuwapa faina wapinzani.

“Tunatakiwa kuongeza umakini katika eneo la hatari, mipira ya kutenga sio mizuri, wachezaji wanatakiwa kuchukuwa thadhari kwa sababu katika mpira lolote linaweza kutokea na tusiruhusu kufunga.

Tumepata matokeo mazuri kwenye mechi ya kwanza lakini hatulazimiki kuridhika yaliyopita na anaimani El Merrikh wataingia kivingine kwa sababu ya wao kutaka kupata matokeo,” alisema Kocha huyo.

Alisisitiza kuwa walifanikiwa kupata mabao 2-0 ugenini, anatarajia hata wapinzani wao wana uwezo wa kushinda wasipokuwa makini wachezaji na kuruhusu wakacheza na kufanya mashambulizi.

Gamond alisema wanahitaji matokeo mazuri katika mechi hiyo kuwafunga na kutowaruhusu El Merrikh kutopata nafasi ya kupata matokeo ambayo watakosa kuingia hatua ya makundi.

SOMA NA HII  SERENGETI BOYS WAPAA KWENDA MOROCCO KWENYE MICHUANO YA AFCON U-17