Home Azam FC WAKATI SIMBA NA YANGA ZIKIWA ‘BIZE’ NA CAF…AZAM BADO WAKOMAA NA USAJILI...

WAKATI SIMBA NA YANGA ZIKIWA ‘BIZE’ NA CAF…AZAM BADO WAKOMAA NA USAJILI MPYA…

Habari za michezo leo

KLABU ya Azam imetuma maombi rasmi ya kumuhitaji kipa wa Tabora United Mnigeria, John Noble kwa ajili ya kukitumikia kikosi hicho wakati dirisha dogo la usajili litakapofunguliwa Desemba 16.

Taarifa kutoka ndani ya timu hiyo zinasema ni kweli mawasiliano baina ya viongozi hao yamefanyika huku Tabora ikiwa tayari kumuachia ikiwa tu itampata mbadala wake.

“Kutokana na dirisha kufungwa ila mazungumzo baina yetu (Azam) na wao (Tabora) yanaendelea kwa ajili ya kumpata kipa huyo,” kilisema chanzo hicho.

Kwa upande wa Ofisa Mtendaji Mkuu wa Tabora United, Thabit Kandoro alisema anachofahamu yeye ni mkataba wa miaka miwili uliopo baina yao na mchezaji hivyo hayo mengine hawezi kuyazungumzia.

“Noble ana mkataba wa miaka miwili na tumesikia baadhi ya timu zimeanza kumlaghai zikimuhitaji, sisi hatuhangaiki na hilo bali tutasimamia katika makubalino ya kimkataba tuliyoingia,” alisema.

Noble mwenye uzoefu mkubwa na soka la Afrika amejiunga na timu hiyo msimu huu akitokea Enyimba ya kwao Nigeria huku akiwahi pia kuichezea ASC Kara ya Togo aliyoitumikia 2020.

Sababu kubwa za Azam kumuhitaji Noble ni kutokana na kipa namba moja, Mghana, Abdulai Iddrisu kutoelewana na na Kocha wa Makipa, Khalifa Ababakar Fall.

SOMA NA HII  KAZI IMEANZA ...RASMI YANGA YAANZA MAZUNGUMZO NA CHAMA..MORRISON AANDALIWA MKATABA...