Home Habari za michezo WAKATI AL AHLY WAKIICHORA SIMBA KWA ‘DARUBINI’…KAPOMBE KAWACHEKI WEE..KISHA AKASEMA HILI..

WAKATI AL AHLY WAKIICHORA SIMBA KWA ‘DARUBINI’…KAPOMBE KAWACHEKI WEE..KISHA AKASEMA HILI..

Habari za Simba

BEKI wa Simba, Shomary Kapombe amesema ushiriki wa timu hiyo katika michuano ya African Football League yatazidi kuifanya timu hiyo iwe bora zaidi kimataifa na kama wachezaji wamejiandaa kufanya kweli.

Simba imepangwa dhidi ya Al Ahly ya Misri katika mechi ya ufunguzi wa michuano hiyo mipya, inayoshirikisha pia Esperance (Tunisia), Wydad Casablanca (Morocco), Mamelodi Sundowns (Afrika Kusini), Enyimba (Nigeria), TP Mazembe (Congo) na Petro Atletico (Angola).

“Michuano hii ni mikubwa, sio kwa timu hata kwa wachezaji tumeingia katika historia ya kipekee kuanza kuicheza na bahati kubwa Simba imeingia ikiwa kati ya klabu nane Afrika, tunaendelea kujipanga maana ushiriki wetu utatufanya kufanya vizuri zaidi katika michuano mingine ambayo timu itashiriki,” alisema

Pia, alisema wachezaji wote wanaufahamu ubora wa Al Ahly na ukubwa wake hivyo ni moja ya kipimo kizuri kwa wachezaji.

“Tutaendeleza historia yetu ya Kwa Mkapa hatoki mtu, maana tunajivunia wingi wa mashabiki wetu, tutahakikisha tunapambana kufanya vizuri katika michuano hii,” alisisitiza Kapombe aliyekuwa walipoizamisha Al Ahly kwa bao 1-0 katika mechi za makundi ya Ligi ya Mabingwa 2020-2021 kwa bao lililofungwa na Luis Miquissone ambaye baadaye alinunuliwa na klabu hiyo.

SOMA NA HII  IKAMATE SHAOLIN POWER YENYE USHINDI MPAKA MARA 2000 YA DAU LAKO KUPITIA MERIDIANBET..