Home Habari za michezo KUHUSU ISHU YA KUSAFIRISHA MASHABIKI….PRIVALDINHO ‘AMLIPUA VIBAYA’ AHMED ALLY…

KUHUSU ISHU YA KUSAFIRISHA MASHABIKI….PRIVALDINHO ‘AMLIPUA VIBAYA’ AHMED ALLY…

Habari za Michezo

Msimamizi wa Maudhui ya Mitandaoni (Digital Manager) ya Klabu Bingwa Tanzania Bara Young Africans Priva Abiudi Shayo ‘Privaldinho’ amemjibu Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Simba, Ahmed Ally ambaye aliyesema Yanga wamemuiga yeye kusafirisha mashabiki nje ya nchi.

“Wanahaha, Mzee Luis Sendeu alisafiri sana na mashabiki na mabasi. Jerry Murro alisafirisha kombe na mashabiki hadi Rwanda (2012).

“Antonio Nugaz alisafiri na mashabiki kwa basi kwenda Ndola (vs Zesco) 2018.

“Mfikirwa na mimi tulienda Dr Congo na mashabiki kwa basi. Huyo nae (Ahmed) kipindi cha nyuma kasafiri sana na mabasi yetu sasa sijui anasema tumeiga nini,” amesema Priva.

SOMA NA HII  WAKATI YANGA WAKIMRUDISHA KISINDA BONGO...CHAMA KAWATAZAMA WEE...KISHA KWA 'ZARAU' AKAWAAMBIA HAYA...