Home Habari za michezo BAADA YA KUWASUMBUA ZAMBIA…MABOSI SIMBA WAULIZIA MKATABA WA WINGA ‘KISHADA’…

BAADA YA KUWASUMBUA ZAMBIA…MABOSI SIMBA WAULIZIA MKATABA WA WINGA ‘KISHADA’…

Tetesi za Usajili Simba

Uongozi wa Simba SC umeanza mazungumzo na winga wa Power Dynamos ya Zambia, Joshua Mutale kwa ajili ya kumsajili katika dirisha dogo msimu huu.

Winga huyo alikuwa mwiba katika goli la Simba SC walipokutana Jumamosi (Septemba 16) kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Barani Afrika, huku akitengeneza nafasi ya bao la kwanza kwa timu yake.

Timu hizo zilivaana kwenye Uwanja wa Levy Mwanawasa mjini Ndola, Zambia ambapo zilitoka sare ya mabao 2-2.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Zambia, mmoja wa mabosi wa timu hiyo, mwenye ushawishi wa usajili amemfuata winga huyo kwa ajili ya kufanya naye mazungumzo, na kikubwa kutaka kufahamu ukomo wa mkataba wake ndani ya Power Dynamos.

Mtoa taarifa huyo amesema mara baada ya kuuliza ukomo wa mkataba wake, mchakato wa kufanikisha mazungumzo ya kumsajili winga huyo umeanza baada ya Kocha Mkuu wa Simba, Mbrazili, Roberto Oliveira ‘Robertinho’ kuvutiwa naye.

“Mara baada ya mchezo kumalizika dhidi ya Power Dynamos, haraka mmoja wa viongozi wetu alimfuata Mutale kwa ajlili ya mazungumzo ya awali na winga huyo.

“Uongozi na benchi la ufundi wamevutiwa na kiwango chake katika mchezo tuliocheza dhidi ya Power Dynamos, hivyo kama mazungumzo yatakwenda vizuri basi huenda akapewa mkataba mapema wakati akisubiria usajili kufunguliwa.

“Uzuri ni kwamba benchi la ufundi lenyewe limevutiwa naye, kama unavyofahamu bado timu ina tatizo la winga mwenye kasi, hivyo huyo Mutale anatosha kabisa,” amesema bosi huyo.

SOMA NA HII  KAMATA 'MAOKOTO' YA UHAKIKA KUPITIA SLOT YA BLACK GOLD NDANI YA MERIDIANBET...

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here