Home Habari za michezo KUHUSU HESHIMA YA SIMBA,BENCHI LA UFUNDI LIMEKUJA NA KAULI HII

KUHUSU HESHIMA YA SIMBA,BENCHI LA UFUNDI LIMEKUJA NA KAULI HII

Habari za Simba

Benchi la ufundi la Simba SC umetoa maagizo mapya kwa wachezaji wa klabu hiyo wakiongozwa na washambuliaji wao hatari, Luis Miquissone na Jean Baleke kuhakikisha kuwa wanafika mbali.

Simba SC wanaanza michuano ya kimataifa msimu huu wakiwa kwenye hatua ya pili ambapo watakipiga dhidi ya Mabingwa wa Soka nchini Zambia Power Dynamos mwishoni mwa juma lijalo (Septemba 16) mjini Ndola katika Uwanja wa Lavy Mwanawasa.

Meneja wa ldara ya Habari wa Simba SC, Ahmedy Ally amesema kuwa tayari wamewapa meseji wachezaji wa Simba SC kuwa wanadeni kubwa la kuhakikisha kuwa wanafika mbali kwenye michuano yote ambayo watashiriki msimu huu.

“Wachezaji tayari wamepewa maagizo yao kuwa wanadeni kubwa la kuhakikisha Simba SC inafika mbali katika michuano hii ya kimataifa, jambo kubwa ambalo lipo ni kuonani kwa kiasi gani wanafahamu kuwa Simba SC katika kila msimu lazima ifike hatua ya makundi na kisha Robo Fainali na msimu huu tunaitaka Nusu Fainali.

“Hilo ni jambo ambalo linaeleweka Simba SC linapokuja suala la michuano ya kimataifa, basi inatakiwa kuheshimiwa na wachezaji kutuheshimisha na tunaamini watatupa heshima hiyo katika michuano yote msimu huu” amesema Ahmedy Ally.

SOMA NA HII  ACHA KUZUBAA....NAFASI YA KUWA TAJIRI USIKU LEO HII HAPA KUPITIA DEUCES WILD YA MERIDIANBET...