Home Habari za michezo SIMBA vs COASTAL UNION: MECHI ILIYOISHA KABLA YA KUCHEZWA…TARAJIA KUYAONA HAYA…

SIMBA vs COASTAL UNION: MECHI ILIYOISHA KABLA YA KUCHEZWA…TARAJIA KUYAONA HAYA…

Simba SC vs Coastal Union

NYASI za uwanja wa Chamazi kesho zitawaka moto kwenye mechi ya Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba inakuwa wenyeji ikiwakaribisha Coastal Union.

Simba anahitaji kupata matokeo kuendelea kujiimarisha katika malengo yao wakiwa nafasi ya nne akiwashinda mechi zote mbili wakiwa na alama 6, kwenye mchezo wa leo wanahitaji kupata alama tatu kujiimarisha zaidi kwenye safari yao ya kutaka kuwania taji la ubingwa wa ligi hiyo.

Kwa upande wa Coastal Union nao wanaingia kusaka alama ili kujiondoa kwenye nafasi ya chini wakiwa nafasi ya 14 baada ya kucheza mechi mbili akipoteza moja na sare moja akiaa na alama moja.

Kuelekea mchezo huo, Kocha wa Simba, Roberto Oliviera ‘Robertinho’, alisema wachezaji wake wako tayari kwa mchezo huo baada yakufanya maandalizi mazuri na malengo yao ni kusaka ushindi na kucheza mpira mzuri.

Alisema wanaenda uwanjani sio kucheza bali wanahitaji kufikia malengo yao ya kusaka ushindi na kucheza soka fast ambalo itawapa furaha mashabiki mashabiki wao na kufikia malengo yao.

“Hatuendi uwanjani kucheza tu, tuna malengo yetu na wachezaji kuwa makini na tunatumia vizuri nafasi tunazotengeneza kupata ushindi mnono, tunawaheshimu Coastal Union timu nzuri tutacheza kwa umakini mkubwa ili kufikia kile kinachotarajiwa,” alisema Robertinho.

Aliongeza kuwa baada ya mechi na Power Dynamos ya Zambia, walianza kufanya maandalizi ya mechi ya ligi mapema kwa kuwapa mbinu mpya anaamini ataanza kuifanyia kazi katika mchezo wa leo.

“Hakuna shida kati yangu na wachezaji wote tunawasiliana vizuri iwe kambini na uwanjani kikubwa ninachowaelekeza wachezaji wangu kumuheshimu mpinzani wetu na kuwa makini uwanjani kupambana kwa ajili ya kupata matokeo mazuri,” alisema Kocha Robertinho.

Kocha Msaidizi wa Coastal Union Fikiri Elius alisema wachezaji wake wako vizuri wanaiheshimu Simba timu kubwa na mara zote wanapokutana wanapoteza.

Alisema wanacheza mchezo huo kwa tahadhari kubwa wakitambua ubora wa Simba ulipo, kwa sababu wao wanahitaji matokeo mazuri kutoka kwenye nafasi ya chini waliopo sasa.

“Haitakuwa mechi ya upande mmoja, tumafahamu kuwa Simba ni timu kubwa, ina wachezaji wazuri, tumefanya maandalizi ya kutosha na wachezaji wameendaliwa kwa ajili ya kupambana kupata matokeo chanya kwenye mchezo wa kesho ,” alisema Fikiri.

Mechi ya pili itakayochezwa Azam Complex saa 1:00 usiku, Kocha Mkuu wa Azam FC, Bruno Ferry alisema wanatarajia kupata ushindani kwa sababu ya walivyowaangalia wapinzani wao kwenye mchezo wa kimataifa.

Alisema wameona ubora na changamoto za wapinzani wao na wamejianda kutafuta matokeo ya ushindi ili kufikia malengo yao ya kutwaa taji la ubingwa baada ya kuondolewa mapema kwenye michuano ya kimataifa.

SOMA NA HII  BAADA YA KUONA UCHEZAJI WA 'SURE BOY' AKIWA YANGA..CHUJI AGUNA KISHA AFUNGUKA HAYA...