Home Habari za michezo SIKU CHACHE BAADA YA KUSHINDA KUANDAA AFCON 2027.., WAKENYA WAANZA ‘KUTIFUANA’….

SIKU CHACHE BAADA YA KUSHINDA KUANDAA AFCON 2027.., WAKENYA WAANZA ‘KUTIFUANA’….

Habari za Michezo leo

Macho yanamulikwa nchini Kenya kuhusu utayari wao wa kuandaa michuano ya Kombe la Afrika 2027 suala kubwa likiwa uwepo wa viwanja vyenye viwango vya kimataifa.

Kenya wakishirikiana na mataifa jirani ya Tanzania na Uganda, waliwasilisha ombi la kuwa wenyeji wa Kombe la Afrika kupitia Pamoja Bid ambalo lilikubalika na Shirikisho la Soka Afrika (CAF).

Rais wa CAF, Patrice Motsepe, alipongeza mataifa hayo matatu na hususan Marais William Ruto wa Kenya, Mama Samia Suluhu Hassan wa Tanzania na Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda kwa kuwa mstari wa mbele kusapoti Pamoja Bid.

Tayari Serikali kupitia Wizara ya Michezo imetangaza viwanja vinne vitakavyokarabatiwa kwa ajili ya michuano hiyo mikubwa ya soka barani Afrika ambazo ni Nyayo na Kasarani zote za jijini Nairobi na Kipchoge Keino ya mjini Eldoret, Kaunti ya Uasin Gishu.

Pia Serikali imepanga kujenga uwanja mpya jijini Nairobi utakayofahamika kama Talanta Stadium.

Uamuzi wa michuano hiyo kupelekwa Nairobi na Uasin Gishu umeibua cheche za siasa hususan kwa wanasiasa kutoka kanda za Nyanza na Magharibi wakilalamikia maeneo yao yametengwa wakidai ndiyo ngome ya mashabiki wa soka.

Taarifa ya pamoja ya magavana Profesa Anyang’ Nyong’0 wa Kaunti ya Kisumu na mwenzake wa Kaunti ya Kakamega, Fernandes Barasa, wanaitaika Wizara ya Michezo kufikiria upya uamuzi wao na kuruhusu mechi zipigwe Kakamega na Kisumu.

“Ukanda huu ndiyo walipo mashabiki shakiki wa soka na watajitokeza kwa wingi kujaza uwanja na sio Eldoret ambayo imejizolea umaarufu kuwa na mashabiki wengi wa riadha,” ilisomeka taarifa hiyo ya pamoja.

SOMA NA HII  ACHANA NA 'SIMU MALOPOLOPO'....TECNO WANAKUJIA NA SPARK 10 PRO...MAUJANJA YAKE YOTE HAYA HAPA...