Habari za michezo

KOCHA AFUNGUKA HAYA BAADA YA MANULA KUREJEA KIKOSINI

Staff Desk October 7, 2023 1:33 pm

Wakati mashabiki wa Simba baadhi wakiwa hawana imani na kipa Ayoub Lakred kutokana na kuruhusu mabao katika mechi mbili za kimataifa, tabasamu limeanza kuonekana baada ya Aishi Manula kuanza mazoezi ya uwanjani.

Manula ambaye ni kipa namba moja wa Simba, amerejea kwenye uwanja cha mazoezi mara baada ya kuwa nje muda mrefu akiuguza majeraha ya mguu.

Manula ameanza rasmi mazoezi na magolikipa wenzake ndani ya klabu hiyo tofauti na awali alipokuwa akifanya binafsi kwa takribani wiki tatu.

Kwa mujibu wa duru za habari kutoka kwenye uongozi wa Simba, zinasema kuwa Manula kwa sasa yupo tayari kwa ajili ya kukaa kwenye milingoti mitatu ya Simba.

Kocha wa Makipa wa Simba, Dani Cadena, alisema: “Haya ni mazoezi ya nne baada ya kuumia. Nina furaha kwa mabadiliko yanayoonekana kidogokidogo.”

KWA HALI HII YA BOCCO, HAWA JAMAA WATASUBIRI SANA JIPATE WIKIENDI HII NA MERIDIANBET KUPITIA KIPUTE KATI YA ARSENAL DHIDI YA MAN CITY …

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

2 responses to “KOCHA AFUNGUKA HAYA BAADA YA MANULA KUREJEA KIKOSINI”

  1. Geofrey daudi says:

    Nauliza mchezaji wa yanga wa kimataifa Djuma Shabani kwa sasa yupo timu ipi akiitumikia msimu huu 2023/2024

  2. admin says:

    Taarifa tulizonazo ni kuwa mchezaji huyo kasaini mkataba wa awali na Azam FC KWA AJILI YA MSIMU UJAO

Leave a Reply