Home Habari za michezo WALIOIKAZIA YANGA MBEYA ..WAKUNG’UTWA DAR….

WALIOIKAZIA YANGA MBEYA ..WAKUNG’UTWA DAR….

Habari za Michezo leo

IHEFU SC imeshindwa kushikilia bomba baada ya jioni hii ikiwa jijini Dar es Salaam kupigwa bao 1-0 na KMC katika mfululizo wa mechi za Ligi Kuu Bara, ikiwa ni siku chache tu tangu itoke kuitoa nishai Yanga kwenye Uwanja wa Highland Estate, jijini Mbeya.

Timu hiyo iliifumua Yanga mabao 2-1 na kuitibulia rekodi ya kushinda mechi mfululizo za ligi ikirudia kile ilichokifanya msimu uliiopita ilipoitibuliwa rekodi ya kucheza mechi 49 bila kupoteza baada ya kuifunga pia idadi kama hiyo katika mechi iliyokuwa ya 50 kwa Yanga ikisaka kuendea kufunika Bara.

Hata hivyo, ikiwa kwenye Uwanja wa Uhuru, Ihefu ilikubali kichapo cha bao 1-0, lililowekwa kimiani dakika ya 58 na Ibrahim Elias na kuifanya isaliwe na alama zao sita baada ya mechi tano ilizocheza.

Matokeo hayo yamekuwa muendelezo mzuri kwa KMC kwani ni mchezo wa tatu mfululizo kushinda baada ya awali kuifunga JKT Tanzania na Geita Gold kwa mabao 2-1 kila moja na kuifanya sasa ifikishe pointi 10 na kuchupa kutoka nafasi ya tano hadi ya nne baada ya mechi tano za ligi.

Katika mchezo wa leo, Ihefu ilishindwa kabisa kuonyesha makeke, licha ya kutengeneza nafasi kadhaa kama ilivyokuwa kwa wenyeji ambao walitumia nafasi waliyoipata kujiandikia ushindi huo, wakati ligi ikienda mapumziko kwa muda wa kama wiki mbili.

SOMA NA HII  GAMONDI AMUA KUFANYA KWELI LIGI YA MABINGWA