Habari za michezo

KUHUSU MCHEZAJI BORA WA MWEZI YANGA MCHAKATO UKO HIVI

Staff Desk October 9, 2023 4:19 pm

Klabu ya Yanga leo imesaini mkataba na Shirika la Bima la Taifa ‘National Insurance Cooperation’ kuwa mdhamini wa Mchezaji Bora wa Mwezi (NIC Player of the Month).

Mkataba huo ni wa miaka mitatu (3) wenye thamani ya Tsh milioni 900 (sawa na Tsh milioni 300 kwa mwaka).

Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano Yanga, Ally Kamwe amesema kuwa mchezaji Bora wa Mwezi atapatikana kutokana na kura za mashabiki wa klabu hiyo.

“Utaratibu ambao utatumika kumpata Mchezaji Bora wa Mwezi, jopo la ufundi la Yanga litatangaza wachezaji watatu ambao watapigiwa kura na mashabiki/wapenzi ili kumpata mshindi.”

“Zoezi la kumtafuta Mchezaji Bora wa Mwezi wa Yanga [NIC Player of the Month] litaanza rasmi mwezi huu (Oktoba, 2023),” amesema Ally Kamwe.

KABLA YA KIMATAIFA GAMONDI AWATAKA AZAM KWANZA BAADA YA KUJUA WAPINZANI WAKE CAF….MBRAZILI SIMBA KAGUNA KIDOGO…KISHA AKASEMA HILI…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply