Home Habari za michezo ROBERTINHO AWATETEA MASTAA SIMBA KISA USHINDI HUU

ROBERTINHO AWATETEA MASTAA SIMBA KISA USHINDI HUU

Habari za Simba SC

Kocha Mkuu wa Simba SC, Roberto Oliviera ‘Robertinho’ amewatetea wachezaji wake kwa kushinda mchezo dhidi ya Singida FG wakiwa na uchovu wa safari na mechi mfululizo.

Robertinho ametoa kauli hiyo leo Oktoba 8, 2023 mara baada ya kuifunga Singida 2-0 katima dimba la CCM Liti mkoani Singida.

“Kipindi cha kwanza tumecheza vizuri na lazima niwapongeze wachezaji wangu wametoka kucheza mechi mfululizo, uchovu wa safari lakini tumepata alama tatu,” alisema Robertinho.

Kwa ushindi huo, Simba wamekwea kileleni kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya NBC kwa kufikisha alama 15, wakifuatiwa na Azam FC wenye alama 13 huku wapinzani wao Yanga wakiwa nafasi ya tatu na alama zao 12.

SOMA NA HII  RAISI SAMIA AWAKOSHA WADAU WA MICHEZO SIMBA DAY, AFUNGUKA KUHUSU GOLI LA MAMA, KUJUSU UJENZI WA VIWANJA ISHU IKO HIVI