Habari za Simba
Habari za michezo

MBABE WA YANGA HAPOI AIBUKIA HUKU

Staff Desk October 18, 2023 12:44 pm

ZUBER Katwila, aliyekuwa kwenye benchi Uwanja wa Highland Estate ubao uliposoma Ihefu 2-1 Yanga anatajwa kuwa katikà hesabu za mabosi wake wa zamani Mtibwa Sugar.
Baada ya kupewa mkono wa asante ndani ya Ihefu Oktoba 14 2023 Nyerere Day kocha huyo alikuwa anatajwa kuibukia ndani ya Singida Fountain Gate.
Dili lake la kuibukia hapo lilikwama baada ya mabosi wa Singida Fountain Gate kumpa kibarua kocha mpra raia wa Brazil Ricardo Ferreira ambaye ameshaanza majukumu yake.
Mtibwa Sugar haijawa katika mwendo mzuri ñdani ya msimu wa 2023/24 kwenye mechi tano haijaambulia ushindi zaidi ya sare mbili zilizoipa pointi mbili.

Katwila amepewa mkono wa Asante ñdani ya Ihefu hivyo muda wowote kuanzia sasa atakuwa katika changamoto mpya ikiwa makubaliano yatakuwa sawa pande zote

JAMBO LISIWE GUMU MASTAA SIMBA WAJAZWA MINOTI MAPEMA AFL DHIDI YA AL AHLY YANGA VS AZAM SIO POA KWA HALI HII LOLOTE LINAWEZA KUTOKEA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply