Usajili wa Yanga 2026/27
Yanga SC

Hersi Said Afunguka Usajili wa Yanga 2026/27: “Bado Mchezaji Mmoja!”

Vardo August 2, 2026 11:13 pm

RAIS wa Yanga SC, Injinia Hersi Said, amefunguka sababu zilizofanya uongozi wa klabu hiyo kufanya usajili mkubwa na wa kishindo kuelekea msimu mpya wa 2026/27, huku akitoa taarifa mpya itakayowasisimua wanachama na mashabiki wa Wananchi.

Hersi amebainisha kuwa kabla ya dirisha la usajili kufungwa rasmi, Yanga itamtambulisha mchezaji mmoja zaidi ili kukamilisha safu yao ya ushindani.

Somo la Msimu Uliopita Laisukuma Yanga

Akizungumza kuhusu maandalizi ya msimu huu, Hersi alisema uzoefu na changamoto walizopitia msimu uliopita ziliwapa somo kubwa, jambo lililowapa msukumo wa kufanya maboresho makubwa kwenye kikosi ili kuwa na ushindani wa kweli katika kila nafasi.

Alikiri kuwa, licha ya kuhudhuria mechi mbalimbali za timu hiyo, mara nyingi hakuwa na amani kutokana na mapungufu yaliyokuwa yakionekana uwanjani.

“Tumefanya usajili mkubwa sana msimu huu kwa sababu hatutaki kurudia makosa yaliyotokea msimu uliopita. Nilikuwa naenda kuangalia mechi zetu lakini sikuwa na amani kabisa. Safari hii tumefanya maandalizi ya kutosha kuhakikisha timu inakuwa imara na yenye uwezo wa kushindana katika kiwango cha juu,” alisema Hersi.

Mshangao Mwingine Unakuja Wananchi!

Akiwatoa hofu mashabiki wa Yanga, Hersi amesisitiza kuwa shughuli ya usajili bado haijakamilika kwa 100% upande wao. Kuna ingizo jipya linalosubiriwa kutambulishwa muda wowote kuanzia sasa kabla ya siku ya mwisho ya usajili.


Rekodi za Kuitisha za Hersi Said Yanga SC (Miaka 4)

Katika hatua nyingine, Rais Hersi alieleza mafanikio makubwa ambayo uongozi wake umeyapata katika kipindi cha miaka minne iliyopita kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara na mashindano mengine:

  • Mechi za Ligi Kuu: Mechi 120 (Ushindi: 101, Sare: 12, Kupoteza: 7 pekee).

  • Pointi: Pointi 315 zilizokusanywa.

  • Mabao: Yanga imefunga mabao 286 na kuruhusu mabao 51 pekee (Tofauti ya mabao +235).

  • Mataji: Makombe 16 ya ndani na nje ya nchi, ikiwemo mataji 4 mfululizo ya Ligi Kuu Tanzania Bara (sehemu ya rekiodi ya kutwaa ubingwa mara 5 mfululizo).

Zuchu Na Diamond Wampata Mtoto Wa Kike: Bi Sandra (Mama Dangote) Apewa Heshima Kubwa! Bodi ya Simba SC Yatengua Maamuzi ya Bunju: Kikao Kizito Kutajwa Kesho