Habari za Simba SC
Habari za michezo

TRY AGAIN AWAKUMBUSHA WATANZANIA JAMBO HILI MUHIMU SIMBA VS AL AHLY

Staff Desk October 18, 2023 6:59 pm

Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi wa Klabu ya Simba, Salim Abdallah ‘Try Again’ amesema kuwa mchezo wao wa robo fainali ya African Football League (AFL) dhidi ya AL Ahly sio mchezo wa Simba pekee bali Taifa zima la Tanzania.

Try Again amesema hayo kuelekea mchezo huo utakaopigwa keshokutwa Ijumaa, Oktoba 20, 2023 katika Dimba la Mkapa jijini Dar es Salaam.

“Tunafahamu Al Ahly ni timu kubwa, ni mabingwa wa Afrika, tunawaheshimu. Lakini Simba sio wadogo, ni miongoni mwa klabu nane [8] bora Afrika, kwa hiyo tunao uwezo wa kupambanao na kupata matokeo.

“Nawaomba watanzania hii ni mechi ya watanzania wote sio mechi ya Simba, kwa hiyo nawaomba watanzania waje kwa wingi uwanjani kuiunga mkono timu yao ya Simba ambayo itakuwa inaiwakilisha Tanzania.

“Kwa hiyo wanunue tiketi waje uwanjani, nilikuwa naangalia mauzo ya tiketi tayari tumevuka 60%. Watu waje kuangalia burudani za ufunguzi wa mashindano haya ambayo imeandaliwa kwa kiwango cha zaidi ya sherehe za AFCON,” amesema Salim Abdallah.

RAIS WA YANGA KUTOKA JANGWANI MPAKA KILELE CHA KILIMANJARO SIMBA: AL AHLY ANAKUFA….BOSI AFUNGUKA MPANGO MZIMA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply