Habari za Simba
Habari za michezo

BOCCO ATAMBA NYUMBANI MATOKEO MAZURI UHAKIKA

Staff Desk October 19, 2023 3:58 pm

Ni mchezo mkubwa kwa Tanzania na Afrika kwa ujumla, utakuwa mchezo mzuri sana. Ni nafasi nzuri kwa klabu yetu na sisi wachezaji kuonesha kiwango kizuri katika mchezo huo na mashindano haya makubwa.

Tunatarajia kuonesha mchezo mzuri na wa kiungwana kwa wapinzani wetu ingawa tunajua utakuwa mchezo mgumu kwa sababu tunakutana na timu kubwa yenye wachezaji wazoefu kwenye mashindano kama haya.

Tuna imani tuna timu nzuri na wachezaji wenye uzoefu wa mechi kama hizi, tunatarajia matokeo mazuri kwa sababu tunacheza nyumbani halafu ni mchezo wa kwanza kwenye mashindano ya mtoano.

Ni kitu kikubwa na cha kujivunia kama nchi kupata nafasi ya kuandaa mechi ya ufunguzi wa mashindano haya makubwa, wachezaji tuna jukumu kubwa la kupata matokeo mazuri uwanjani kwa sababu ni mchezo wa kwanza na tunacheza nyumbani.

BOCCO, MBRAZILI WAIPIGA BITI LA KUFA MTU AL AHLY …. MASTAA YANGA WAFUNGUKA MAGUMU HAYA WANAYOPITIA LIGI KUU

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply