Habari za Simba
Habari za michezo

BAADA YA ZIMBWE Jr KUMPELEKEA ‘MOTO’ JANA…TAU KATIKISA KICHWA WEE..KISHA AKASEMA HILI..

admin October 21, 2023 7:39 pm

Mchezo wenye hadhi ya ufunguzi wa michuano mipya ya African Football League (AFL) Simba dhidi ya Al Ahly umemalizika kwa sare ya mabao 2-2.

Baada ya mchezo huo kocha Mkuu wa Simba Roberto Oliveira amesema ameridhishwa na kile kilichofanywa na wachezaji wake kwenye mchezo huo kwani wameweza kutoka nyuma na kuuchukua mchezo.

Robertinho amesema anaamini chochote kinaweza kutokea katika mchezo wa mkondo wa pili utakaopigwa nchini Misri.

Kwa upande wake kiungo mshambualiaji wa Simba Saido Ntibazonkiza amesema wachezaji wamefanya kila ambacho walipaswa kukifanya na bado wanaaamini wana uwezo wa kuiondosha Al Ahly kwenye michuano hiyo mikubwa kwa ngazi ya Vilabu Afrika.

Nyota wa Al Ahly Percy Tau amesema ameridhishwa na matokeo ya mchezo huo kwani Simba walirudi imara zaidi kwenye kipindi cha pili.

Kwa matokeo hayo Simba ili itinge nusu fainali ya AFL inahitaji ushidi wa aina yoyote nchini Misri au sare ya kuanzia mabao matatu.

AFRICAN FOOTBALL LEAGUE ….MECHI YA KESHO TP MAZEMBE vs ESPERANCE HAKUNA KIINGILIO… MRITHI WA MAYELE YANGA LAMKUTA JAMBO…..UKAME WATISHIA HATMA YAKE JANGWANI…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply