Habari za Simba SC
Habari za michezo

MASHABIKI SIMBA WAMUANGUKIA KIBU

Staff Desk October 21, 2023 1:07 pm

Jitihada kubwa za kulisakama lango la Al Ahly katika mchezo wa jana zilikuwa zaidi miguuni mwa mshambuliaji Kibu Denis aliyefunga bao la kusawazisha.

Ulikuwa mchezo mkali na wa kusisimua Simba wakiwapelekea pumzi ya moto wapinzani wao hasa kipindi cha pili baada ya kurejea kutoka mapumziko na kumuingiza Jean Baleke na Kanoute.

Baadhi ya mashabiki wa Simba wameanza kumuelewa Kibu kwa sasa baada ya kuonekana si chochote si lolote huko nyuma ambapo kupitia mtandao wa Instagram baadhi ya mashabiki wamefunguka haya;

Nasri Monka amesema; “Mwanangu Kibu tunakuomba utusamehe sana sisi tuliokukatia tamaa, tusamehe ni wakosefu kaka,”

Stephano Yusuph amesema katika kikosi cha Simba kwa sasa Kibu ndiye anayepambana kuhakikisha anakaba na hata kushambulia wengine hawajitumi kama yeye.

Yuhjin amesema; “Natamani wachezaji wote wa Simba wawe kama wewe una kiu kubwa ya mafanikio na mwanzo tulikukataa kabisa tuwie radhi kaka mkandaji,”

Willson Nicky amebainisha kuwa ubora aliokuwa nao taratibu anaanza kuingia kwenye nafsi za wanasimba wengi waliokuwa wakimkataa akiwemo yeye.

“Nashangaa kuona katika wachezaji wanaowania tuzo ya mwezi hayumo mwanangu Kibu, kocha alizingua kumtoa yule Onana anacheza kifather sana,” amesem Nicky

Michael Kisome ameutaka uongozi kuongea na wachezaji waige mfano wa Kibu ambaye ameamua kuwanyamazisha kwa vitendo wote waliokuwa wakimkataa.

MWAMBA HUYU HAPA ALIYEBADILISHA MCHEZO SIMBA vs AL AHLY SARE YA SIMBA vs AL AHLY YAMUIBUA MSIGWA AFUNGUKA KUHUSU GOLI LA MAMA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply