Habari za Simba
Habari za michezo

ROBERTINHO ATOA KAULI YA KIBABE KUELEKEA MECHI YA MARUDIANO

Staff Desk October 22, 2023 8:02 pm

Kocha wa Simba, Roberto Oliveira ‘Robertinho’ wala hana presha na mchezo wa marudiano akiwatumia salamu Al Ahly kuwa wanakwenda kupambana, huku akipangua kikosi.

amesema “Mimi siyo kocha wa kujilinda sijawahi kuwaza kucheza hivyo. Simba itacheza kwa nidhamu kubwa tukitambua ubora wa wapinzani wetu lakini tutawashambulia kwa akili,”

“Tunaweza kuwa na mabadiliko machache ya jinsi ya upangaji wa timu lakini kitu muhimu tutaingia na akili kubwa kupigania heshima ya Simba” amesema na kuongeza,

“Kila mtu ameona mchezo wa juzi. Kama tukiuanza kama tulivyoanza kipindi cha pili kuna kitu tutakitengeneza. Hakuna timu isiyofungika.”

“Kuna makosa tulifanya kipindi cha kwanza. Kuna wakati tulitengeneza urahisi wa Ahly kutushambulia bila sababu za msingi. Nafahamu tulipambana na timu kubwa yenye wachezaji bora lakini tutabadilika.”

Robertinho alikiri kwamba anaweza kuwa na mabadiliko ya kikosi katika mchezo huo utakaopigwa Oktoba 24, jijini Cairo nchini.

Simba inatakiwa kushinda mchezo huo ili iweze kutinga hatua ya nusu fainali.

SIMBA WAJUE MAMBO HAYA KABLA YA KUKUTANA TENA NA AL ALHLY JEZI FEKI ZAIPA HARASA YANGA, MZIGO HUU UMEKAMATWA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply