Habari za Simba
Habari za michezo

MANULA, KRAMO NJE YA DIMBA SIMBA vs AL AHLY

Staff Desk October 23, 2023 3:42 pm

Mlinda mlango wa wa klabu ya Simba Sc, Aishi Manula ‘Air Manula’ na winga Aubin Kramo hawatakuwa sehemu ya kikosi ambacho kitakipiga kwenye mchezo wa marudiano wa michuano ya African Football League dhidi ya Miamba ya Misri na Afrika Al Ahly.

Manula ameshapona majeraha yake lakini hayupo fiti kimchezo japo kuwa ameshaanza mazoezi na wachezaji wenzake huku Kramo bado yupo nchini kwao ambapo alienda kuuguza majeraha yake yaliyokuwa yanamsumbua.

Kwenye orodha ya wachezaji 24 waliosafiri kuelekea nchini Misri majina ya Aishi Manula na Aubin Kramo hayapo hii inaashiria kutokuwepo kabisa kwenye mchezo huo unaotarajiwa kupigwa Oktoba 24 katika dimba la Cairo International.

KWA HILI UNAWEZA KUSEMA OKTOBA NI MWEZI WA YANGA ROBERTINHO AKIFUMUA KIKOSI CHA SIMBA MAPEMA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply