Home Habari za michezo BAADA YA YANGA KUMALIZANA NA AZAM FC JUZI….LEO NI ZAMU YA SINGIDA...

BAADA YA YANGA KUMALIZANA NA AZAM FC JUZI….LEO NI ZAMU YA SINGIDA KULAMBISHWA MWIKO ..?

Habari za Yanga

VINARA wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga inashuka dimba leo kutafuta alama tatu muhimu mbele ya wageni wao Singida Fountain Gate FC, utakaochezwa leo uwanja wa Benjamin Mkapa Dar es Salaam.

Mbali na mchezo huo mechi nyingine Azam FC itawakaribisha Namungo FC katika dimba la Azam, Chamazi na KMC FC atawakaribisha Tanzania Prisons uwanja wa Uhuru jijini.

Katika michezo yote kila mmoja anahitaji alama tatu ili kufikia malengo yao huku Yanga wakihitaji kuendelea kubaki kileleni mwa msimamo wa Ligi hiyo.

Yanga inashuka dimbani ikiwa imeshinda mechi yao dhidi ya Azam FC na Singida Fountain Gate FC nao wakipata alama tatu ugenini dhidi ya Namungo FC keenye uwanja wa Majaliwa, Ruangwa Lindi.

Timu hizo sio mara ya kwanza kukutana, walikutana msimu uliopita mechi ya kwanza Yanga walikuwe wenyeji kwa kushinda mabao 4 -1 mbele ya wageni wao Singida Fountain Gate FC, Novemba 17, 2022.

Na mechi ya marudiano Yanga walikuwa ugenini wakipata matokeo ya mabao 2 -0, mchezo uliopigwa uwanja wa Liti, Singida, Mei 4, mwaka huu katika mchezo wa mzunguko wa pili.

Kuelekea mchezo huo Kocha wa Yanga, Miguel Gamondi alisema Naiheshimu Singida Big Stars ni timu nzuri ingawa imebadili makocha wawili hadi sasa nimekuwa nikiwafuatilia kwa muda mrefu.

“Nimewaona kwenye Michezo mbalimbali ya Ligi Kuu Bara pamoja na Kombe la Shirikisho barani Afrika naamini utakuwa mchezo mgumu maana tumekuwa tukicheza michezo mfululizo.

Napenda kucheza mechi za namna hii sio rahisi kucheza mfululizo michezo mikubwa naamini kesho mashabiki watakuja kwa wingi kutupa sapoti,” alisema Gamondi.

Kwa uoande wa Kocha wa Singida Fountain Gate FC, Ricardo Ferreira alisema baada ya mechi na Namungo FC tukafanya maandalizi mazuri kufanyia kazi mapungufu yetu na wachezaji wako tayari kwa mchezo huo.

“Tumefanikiwa kuona baadhi ya mechi za Yanga, hautakuwa mchezo rahisi kwa sababu kila mmoja tunahitaji alama muhimu, tutacheza kwa nidhamu kubwa ili kutumia mapungufuya wapinzani wetu kutafuta matokeo chanya,” alisema Ferreira.

SOMA NA HII  PAMOJA NA MGUNDA KUANZA VIZURI SIMBA...BARBARA AISHINDWA KUJIZUIA...AANIKA YA MOYONI KUHUSU NAFASI YAKE...