Habari za Yanga SC
Habari za michezo

GAMONDI AWEKA MPANGO YAKE MEZANI DHIDI YA SINGIDA

Staff Desk October 26, 2023 12:34 pm

Kocha Mkuu wa Kikosi cha Yanga, Miguel Gamondi amezungumzia mipango yake kuelekea mchezo ujao wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Singida Fountain Gate.

Mchezo huo umepangwa kuchezwa Ijumaa ya Oktoba 27, 2023 kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam, kuanzia majira ya saa 12:30 jioni.

Akizungumzia mchezo huo, Gamondi amesema, wachezaji walitumia nguvu kubwa katika mchezo uliopita tulioshinda magoli 3-2 dhidi ya Azam, hivyo anatumia siku tatu za maandalizi kuwaweka sawa wachezaji ili kuendelea na malengo ya kukusanya alama tatu.

“Tumetoka kucheza mechi ngumu sana dhidi ya Azam, wachezaji walitumia nguvu kubwa, tunajaribu kuwa na mazoezi mazuri ndani ya siku tatu hizi kuona utimamu wao umefikia wapi.

“Siwezi kusema kama kutakuwa na mabadiliko ya kikosi, hilo litategemea sana tutakachokiona mazoezini. Mechi ya Singida ni ngumu na tunahitaji kuingia kamili ili kuweza kupata pointi tatu,” alisema Gamondi.

KUMBE SIMBA WALITAKA WENYEWE KUTOLEWA NA AL AHLY ALIYELETA JEZI FEKI SIMBA, YANGA KUANIKWA HADHARANI LEO

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply