Habari za Simba SC
Habari za michezo

KIBU KWA SIMBA ATAKIPIGA SANA MWAMBA HUYU HAPA ATIA NENO

Staff Desk October 28, 2023 12:02 pm

Beki wa zamani wa Simba, Boniface Pawasa amewapa ukweli mashabiki wa timu yake wanaomsonya kiungo wao mshambuliaji Kibu Denis akisema jamaa atacheza sana kwenye timu hiyo.

Akizungumza nasi Pawasa alisema kwa jinsi Kibu alivyo na nidhamu ya kutekeleza majukumu yake uwanjani kama ambavyo anaagizwa na makocha wake ataendelea kuwa chaguo la makocha kokote atakokwenda.

Pawasa ambaye kitaaluma ni kocha alisema Kibu amekuwa ni mchezaji anayekubali mabadiliko ya kocha anayompa na kuyatekeleza kwa kiwango kikubwa.

“Watu huwa nawaona hawafurahii kuona Kibu anacheza lakini kuna kitu hawafahamu hakuna kocha ambaye anaweza kumpuuza Kibu hata kama kuna maeneo anafanya makosa,”alisema Pawasa, mmoja wa wachezaji walioacha alama Simba. “Kibu atacheza sana watu hilo wanatakiwa kutambua, nidhamu ya Kibu ndio silaha kubwa ambayo inamtofautisha na wenzake, ni mchezaji ambaye anachukua kwa kiwango kikubwa maelekezo ya kile ambacho kocha anataka akifanye.

“Anapocheza winga na hata waangalie juzi alivyochezeshwa kama mshambuliaji wa kati akitakiwa kuwa na muda mrefu kucheza eneo la hatari bado alifanya hivyo kwa kiwango kikubwa na akafunga bao ambalo kama amefunga mshambuliaji halisi.”

Lakini Pawasa amemshauri Kocha wa Simba Roberto Oliveira ‘Robertinho’ kumrudisha Kibu kucheza kama winga kisha kuanza na mshambuliaji halisi mmoja.

PAMOJA NA KUSAJILIWA KWA MBWEMBWE ZA DUNIA…ONANA NA KONKON BADO SANA…. KUHUSU UCHOVU WA ZIMBWE Jr NA KAPOMBE…MJADALA MKUBWA HUU HAPA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply