Habari za Simba leo
Habari za michezo

ROBERTINHO ANAVYOPITA KWENYE MIFUMO YA GAMONDI

Staff Desk October 29, 2023 12:35 pm

Juzi kocha wa Yanga alilazimika kumpanga Gift Mauya badala Khalid Aucho katika kiungo cha chini. Doctor Aucho ndiye mchezaji muhimu zaidi Yanga, tayari ana kadi mbili za njano na kama jana angeona kadi nyingine basi angewakosa Simba.

Pacha wake katika kiungo, Mudathir Yahya na yeye ilibidi aende benchi mapema ili kumuweka fiti kwa ajili ya mechi ijayo. Kama ilivyo kwa Aucho, unamuhitaji Mudathir bora wakati wote ili kiungo cha Yanga kisogee.

Baada ya kuongoza mabao mawili Yanga waliamua kupunguza kasi ya mchezo. Wakajihami kwa kumiliki mpira, wakapunguza kukimbia ili kutunza nguvu kwa ajili ya mechi ijayo. Kumbuka bado walikuwa na ratiba ngumu sana hadi kufika juzi.

Kama ilivyo kwa Yanga, Simba wamecheza mechi ngumu mfululizo na wametumia nguvu kubwa. Mbaya zaidi hawajapata nafasi ya kubadilisha/kuwapumzisha wachezaji wao wengi.

Ni Henock Inonga pekee ambaye hajacheza ‘panga pangua’ katika kikosi cha Simba na ni kwa sababu ya majeraha.

FUKO LA MIPESA YA MERIDIANBET LEO LIMELALA KWENYE ODDS HIZI ZA USHINDI… TRY AGAIN:- BAADA YA KUMALIZANA NA MBABE WAO JANA….KINACHOFUATA NI WAO SASA KULIA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply