Habari za Simba SC
Habari za michezo

KIBU DENIS MGENI RASMI SIMBA vs YANGA….KIINGILIO CHA ‘MATAJIRI’ CHATANGAZWA…

admin October 30, 2023 3:08 pm

Uongozi wa Klabu ya Simba umeweka wazi kuwa utadhihirisha ukubwa wao kwa kupata ushindi kwenye mchezo wa Kariakoo Dabi dhidi ya Yanga unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa.

Ni Kariakoo Dabi inayotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa ndani ya dakika 90 kwa timu zote kuwania kupata pointi tatu muhimu.

Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba, Ahmed Ally ameweka wazi kuwa wanatambua ushindani utakuwa mkubwa na wapo tayari kwa ajili ya kupata matokeo kwenye mchezo huo.

“Mchezo dhidi ya Yanga utachezwa siku ya Jumapili Novemba 5, 2023 saa 11:00 jioni katika Uwanja wa Mkapa. Ni mechi kubwa kwetu, ni mechi ambayo inakwenda kuonyesha ubora halisi ya mpira wa Tanzania na ushindi wake unaleta tabasamu kwa mashabiki wa timu husika na kupoteza kunaacha majonzi.

“Ni mechi ambayo tunakwenda kuendeleza ubabe kwa watani zetu. Ili tujiridhishe kwamba msimu huu tutafanya vizuri ni kupata ushindi katika mchezo huo. Tunataka tuchukue ubingwa mapema sana, katika hili tunawashukuru Ihefu kwa kutusaidia kazi na sisi tunataka kuendeleza kuweka tofauti ya alama na Yanga,” amesema Ahmed.

Meneja Habari na Mawasiliano wa Simba Sc, Ahmed Ally, ametangaza kuwa, Mgeni rasmi katika mchezo wa Derby ya Kariakoo utakao zikutanisha Simba dhidi ya Yanga siku ya Jumapili Novemba 5, 2023 atakuwa, Mshambuliaji wao Kibu Denis Prosper (Mkandaji).

Kwenye mechi ya mwisho ya Ligi, Kibu aliwafunga Yanga goli lililowapa ushindi wa 2-0. Goli la kwanza alitupia Henock Inonga.

Aidha katika hatua nyingine, Meneja Habari wa Simba, Ahmed Ally amesema kiingilio katika mechi ya ‘Kariakoo Derby’ ni Sh5,000 kwa mzunguko, Orange ni Sh10,000, VIP A 40,000, VIP B Sh30,000, VIP C 20,000 na Platnum Sh150,000 Jumapili Novemba 5 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa saa 11:00 jion

AHMED ALLY:- GAMONDI AJE KWENYE MAZOEZI YA SIMBA …HATUNA JAMBO DOGO SISI… HUU HAPA ‘UCHAWI’ WA AZIZI KI KUWA MOTO MSIMU HUU NDANI YA YANGA….BALAA LAKE SIO POA..

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply