Home Habari za michezo BALOZI WA UINGEREZA ALIVYOWAPA MAUJANJA SIMBA LEO…AHADI YAKE KUBWA NI HII HAPA…

BALOZI WA UINGEREZA ALIVYOWAPA MAUJANJA SIMBA LEO…AHADI YAKE KUBWA NI HII HAPA…

Habari za Simba

NEEMA inazidi kumiminika Simba, baada ya Balozi wa Uingereza nchini Tanzania, David Concar kutembelea klabu hiyo na kujadili na viongozi wa kikosi cha timu hiyo maendeleo ya soka ndani ya Wekundu hao wa Msimbazi.

Balozi huyo aliyeambatana na viongozi wa Simba, akiwemo Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa Simba, Salim Abdallah ‘Try Again’ na kutembelea mazoezi ya timu hiyo kwenye uwanja wa Mo Simba Arena, Bunju.

Try Again alisema ushiriki wa klabu hiyo na kuonyesha kiwango kizuri katika michuano ya kimaitafa ikiwemo Afrika Football League (AFL) imemvutia Balozi kimemfanya balizi kuvutia na kutembelea klabu hiyo.

Alisema ushiriki wa AFL umefungua milango kwa klabu hiyo kupata ugeni wa Balozi huyo na kujadiliana mambo mbalimbali ya maendeleo ya michezo hapa nchini ikiwemo soka la wanawake na vijana.

“Ujio wa Balozi David utaleta neema kwa Simba baada ya kujadiliana maendeleo ya michezo kwa klabu hiyo ikiwemo timu kubwa, soka la vijana na wanawake lakini pia na manufaa ya nchini.

Ninatarajia baada ya ujio wa hapa pia ataendelea kutembelea kwa wenzetu (Yanga) hii ni baada ya kuweka ushabiki pembeni na sasa tukiangalia mustakabali wa soka letu la Tanzania ambalo limepiga hatua,” alisema Try Again.

Naye Balozi David alisema amefurahi kutembelea klabu hiyo, kikubwa ni kuzungumza maendeleo ya mpira wa miguu kwa ngazi ya klabu na Taifa kwa jumla.

Alisema anapenda sana soka amekuwa akifatilia klabu hiyo kuanzia ngazi ya soka la vijana na wanawake kwa kufanya vizuri na kutembelea na kuweza kujadili maendeleo ya soka ikiwemo kukuza soka la vijana.

“Ujio wangu ndani ya klabu hii utasaidia katika program za soka la vijana na wanawake lakini pamoja na kuona klabu hiyo inazidi kuwa kubwa na kufanya makubwa,” alisema David.

Balozi huyo ametembelea timu hiyo katika mazoezi yake ambayo wanajiandaa na pambano la watani wa jadi (Kariakoo Darby) dhidi ya Yanga, utakaochezwa Jumapili hii uwanja wa Benjamin Mkapa Dar es Salaam.

Simba wamedhamiria kuendeleza kutafuta ushindi katika mchezo huo ili kufikia malengo yao ya kutafuta alama za kuwania mbio za ubingwa wa Ligi Kuu Bara.

SOMA NA HII  VIDEO: WAPINZANI WA SIMBA AS VITA NAMNA WALIVYOTUA BONGO, KESHO KAZINI