Uncategorized

HATA YA NYOTA SITA WA SIMBA MIKONONI MWA MBELGIJI, WAWILI HATIHATI KUPIGWA CHINI MAZIMA

admin March 17, 2020 9:42 pm

IMEELEZWA kuwa nyota sita ndani ya klabu ya Simba mikataba yao inakaribia kumeguka huku nafasi za wengine kubaki zikiwa mikononi mwa Kocha Mkuu wa Simba, Sven Vandernbroeck.

Kwa sasa Ligi Kuu Bara ikiwa imesimamishwa kwa muda wa mwezi mmoja kutokana na hofu ya kusambaa ugonjwa wa Corona Simba ni vinara wa ligi wakiwa na pointi 71 kibindoni.

Nyota hao ni pamoja na beki mzawa Yusuph Mlipili, kiungo Hassan Dilunga na Muzamiru Yassin mshambuliaji Rashid Juma, Gerson Fraga raia wa Brazili na mwenzake Santos.


Habari zinaeleza kuwa ni Hassan Dilunga mwenye uhakika wa kuongezewa mkataba ndani ya Simba kutokana na mchango wake msimu huu ambapo ametupia mabao sita na pasi tatu za mabao.

Nafasi za nyota wawili kutoka Brazili inaeleza kuwa ni finyu nao wataungana na Wilker da Silva aliyecheza dakika tatu ndani ya Ligi Kuu Bara mbele ya Kagera Sugar.

CHIRWA NDIO BABA LAO AZAM FC, CIOBA AKERWA NA UBUTU WA SAFU YAKE YA USHAMBULIAJI NYOTA 11 NDANI YA YANGA WAWEKWA KIKAANGONI

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply