Home Habari za michezo BAADA YA KUJUA WAPINZANI WAKE CAF….MBRAZILI SIMBA KAGUNA KIDOGO…KISHA AKASEMA HILI…

BAADA YA KUJUA WAPINZANI WAKE CAF….MBRAZILI SIMBA KAGUNA KIDOGO…KISHA AKASEMA HILI…

Habari za Simba SC

Kocha Mkuu wa Simba, Roberto Oliviera ‘Robertinho’, amefatilia timu anazokutana nazo kwenye hatua ya makundi ya michuano hiyo na kudai kuwa anaamini kikosi kitafanya vizuri licha ya kupangiwa na timu ngumu.

Simba inapangwa pamoja na timu za Wydad Casablanca ya Morocco, ASEC Mimosas (Ivory Coast) na Jwaneng Gallaxy ya Botswana.

Mechi za mzunguko wa kwanza zitakafanyika kati ya Novemba 24-25 ambapo kila timu lazima zikutane mara mbili nyumbani na ugenini, mbili za kwanza zitaingia moja kwa moja kwenye hatua ya 16 bora.

Robertinho alisema Simba ni miongoni mwa timu kubwa kwa Afrika hivyo wanafuraha kucheza mechi ngumu kama hizi za ligi ya Mabingwa Afrika.

“Tuna mikakati mizuri kuelekea mechi hizo katika histori Simba iliwahi kucheza na timu zote, ikiwemo Wydad Casablanca anbayo hapa tulipata matokeo na kwenda kupoteza ugenini.

Kazi kubwa kwa sasa ni kuandaa timu ambayo itapata matokeo mazuri nyumbani na ugenini ili kutafuta alama za kwenda hatua ya robo fainali ya Afrika,” alisema Robertinho.

Alisisitiza kuwa kwenye kikosi chake kina wachezaji wenye kuwango kuzuri na kuipatoa matokeo chanya timu hiyo na kuhakikisha anaendelea kuwasuka vijana wake kupata matokeo mazuri zaidi nyumbabi na ugenini.

Naye mshambuliaji wa Simba, Shaban Chilunda alisema anaifahamu vizuri ligi ya Morocco na Wydad Casablanca ambayo alicheza bao mara tatu akiwa nchini humo msimu wa 2020/2021 akiwa katika klabu ya Maghreb Tetouan.

Alisema alipokuwa kwenye klabu ya Maghreb Tetouan walicheza na Wydad Casablanca mara mbili kaika ligi ya Morocco na moja katika michuano ya Shirikisho, wanafahamu vizuri na anaimani hawatakuwa wanyonge kwa sababu timu zote zinajuana.

“Ninaimani ni kundi ngumu kwa sababu ukiangalia timu zote zimekuwa na historia na Simba kwa kuwa waliwahi kucheza nazo, ikiwemo msimu uliopita na Wydad Casablanca tuliwafunga hapa na kwenda kututoa kwao.

“Ninaimani Wydad Casablanca na timu ambazo tunakutana nazo kundi moja inaifahamu vizuri Simba kwa hiyo hatutakuwa wanyonge kwa sababu ya ukubwa wetu na wao wanatufatilia kulingana na ubora wa mashindano haya,” alisema Chilunda.

Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa Simba, Salim Abdallah, ‘Try Again’, alisema hakuna hakuna kundi rahisi na anaimani timu walizopangiwa ni saizi yao kwa sababu ya ubira wa wapinzani wao.

Alisema kundi hilo timu zote wameshakutana nazo na zina historia na Simba ikiwemo Jwaneng Gallaxy iliwatoa kwenye mashindano na wamedhamilia hili halijirudii kwa mara nyingine na kuhitaji kulipa kusasi.

“Wydad Casablanca tulicheza nao msimu uliopita tukashinda nyumbani bao 1-0 ugenini kupoteza 1-0 na jumla kuwa sare ya 1-1 lakini tuliondolewa kwa mikwaju ya penati 4-3.

“Kuhusu Ase Mimosas nao tuliwahi kucheza nao tukashunda nyumbani 3-0 matokeo hayo kujirudia kwenye mchezo wa marudiano, kutokana na matokeo ya awali hatutaki kufanya makosa na tunahitaji kufanya vizuri, “ alisema Try Again

SOMA NA HII  AHMED ALLY : KAGERA SUGAR LAZIMA WAPITIE MACHUNGU TULIYOKUTANA NAYO KWAO KAITABA...