Home Habari za michezo DEWJI:- NIMECHOSHWA NA ROBO FAINALI KILA MSIMU…

DEWJI:- NIMECHOSHWA NA ROBO FAINALI KILA MSIMU…

Habari za Simba SC

Aliyekuwa mfadhili wa Simba SC, Azim Dewji ameiomba klabu hiyo kuhakikisha msimu huu wanafika hatua ya Nusu Fainali au Fainali katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika.

Jumapili (Oktoba Mosi), Simba SC ilitinga hatua ya makundi ya michuano hiyo ikiwa ni mara ya tano, kitu ambacho Dewii ameeleza kuwa hilo ni jambo la kawaida kwao kwa sasa na hakuna kipya cha zaidi.

“Niupongeze uongozi wa Simba SC kwa jitihada za kujenga timu imara na mazoea ya kufika Robo Fainali kwa misimu mitano iliyopita kwenye mashindano ya CAF (Shirikisho la Soka Afrika), lakini kwa uzoefu waliokuwa nao nadhani msimu huu wanapaswa kufika mbali zaidi na ninaamini uwezo huo wanao,” amesema Dewji.

Amesema ingawa anatambua ugumu uliopo kwenye michuano hiyo lakini kwa uzoefu walionao anaamini hakuna kinachoshindikana, kikubwa ni kuwepo kwa mikakati mizuri ya uongozi na benchi la ufundi na wachezaji kutimiza majukumu yao ipasavyo.

Wekundu hao wa Msimbazi walifanikiwa kutinga makundi baada ya sare ya bao 1-1 dhidi ya Power Dynamos ya Zambia kwa faida ya mabao ya ugenini baada ya mchezo wa awali wa ugenini kuisha kwa sare ya mabao 2-2.

SOMA NA HII  ISHU YA 'SURE BOY' NA YANGA ...UKWELI WA JAMBO UKO HIVI....