Home Habari za michezo EDO KUMWEMBE:- SIMBA WALIPASWA KUFUNGWA GOLI 4-0 NA AL AHLY JUZI…

EDO KUMWEMBE:- SIMBA WALIPASWA KUFUNGWA GOLI 4-0 NA AL AHLY JUZI…

Habari za Simba

Mchambuzi nguli wa masuala ya soka nchini, Edo Kumwembe amesema kuwa mechi ya ufunguzi ya michuano ya African Football League, mpaka dakika 45 za kipindi cha kwanza, Simba SC walitakiwa wawe wamefungwa mabao 4 na Al Ahly kutokana na makosa waliyokuwa wakiyafanya.

Mchezo huo wa robo fainali ya AFL ulipigwa katika Dimba la Mkapa, Ijumaa iliyopita, Oktoba 20, 2023 na kumalizika kwa sare ya bao 2-2 ambapo leo Oktoba 24, timu hizo zitacheza mchezo wa marudiano katika Dimba la Cairo nchini Misri.

“Mpaka mapumziko Simba ilikuwa wawe nyuma kwa mabao manne. Kwenda mapumziko huku wakiwa wamefungwa bao moja ilikuwa ni jambo la kushangaza.

“Simba ilikuwa iwe imefungwa mabao mengi zaidi na haikuwa sababu ya ubora wa Ally Salim bali Al Ahly walikuwa wanakosa mabao wao wenyewe bila sababu zozote za Msingi”

“Inawezekana hakuna mtu aliyepiga pesa nyingi weekend iliyopita kama ‘Mganga wa Simba’.Unajiuliza ilikuwaje Al Ahly wakawa wanakosa mabao yale? Inashangaza na lazima mganga atakuwa amejisifu sana,” amesema Edo Kumwembe.

SOMA NA HII  MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA CHAMPIONI IJUMAA