Home Habari za michezo KUELEKEA MAKUNDI YA CAF….ENG HERSI ‘AILIA YAMINI’ YANGA….

KUELEKEA MAKUNDI YA CAF….ENG HERSI ‘AILIA YAMINI’ YANGA….

Yanga SC

Rais wa Klabu ya Yanga, Eng. Hersi Said amesema kuwa timu yao imekwenda kwenye hatua ya Makundi ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, si kwa bahati mbaya bali ni kutokana na mipango waliyoiweka.

Hersi amesema kuwa Yanga inakwenda kupambana kwenye michuano hiyo ili kufikia hatua kubwa na kuweka alama na heshima na si kushiriki tu kama ambavyo vilabu vingi vimekuwa vikifanya.

“Tunamshukuru Mungu kwa kupata mafanikio haya, mimi kwangu ninaita ni mafanikio kwa sababu hatujawahi kufikia hii hatua kwa miaka mingi.

“Miaka 25 sio michache na huwezi kukimbia takwimu, ndio uhalisia. Mwaka 1998 ndiyo ilikuwa mara ya mwisho kwa Yanga kutinga makundi ya CAFCL na sasa ni mwaka 2023, hesabu huwa hazidanganyi.

“Tusijipe ufahari kwa kusema ni jambo dogo, hapana, ni jambo kubwa kuingia makundi. Sisi tunataka twende sehemua ambayo tukishiriki kwenye hayo mashindano tunaweka jitihada ili tufanikiwe.

“Hatua ya makundi ambayo Yanga imeingia inaweza kuwa tofauti na uhalisia wa kawaida wa watu ambao huwa wanashiriki mara nyingi. Tunakwenda kupigana kuweka alama pale kwa ajili ya mafanikio na sio kushirki, tunakwenda kushindana,” amesema Eng. Hersi.

SOMA NA HII  TARIMBA AITAJA SIMBA KWA HILI WAKATI SportsPesa WAKISAINI MKATABA NA YANGA...