Home Habari za michezo MJUMBE WA BODI AFICHUA DATA ZA SIMBA KWA WAARABU….UKWELI NA ISHU NZIMA...

MJUMBE WA BODI AFICHUA DATA ZA SIMBA KWA WAARABU….UKWELI NA ISHU NZIMA IKO HIVI…

Habari za Simba leo

Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi Simba SC, Issa Masoud amefanya mahojiano na Egyptian TV kujua wao kama Simba SC wamejiandaaje kwa maana ya maandalizi ya Ufunguzi pamoja na timu yao itakayocheza dhidi ya Al Ahly Oktoba 20, Benjamin Mkapa.

Issa Masoud amesema:

“Timu inajiandaa vizuri na wachezaji wanaendelea na mazoezi na sisi kama Simba SC tunajua tunakutana na timu kubwa yenye historia kubwa Afrika, lakini tofauti na zamani, zamani ilikuwa ukikutana na timu kama Al Ahly mnakuwa wanyonge ila sasa hivi imekuwa ni kinyume maana inakuwa kama hamasa au shauku kwa sababu ni kipimo cha aina ya timu ambayo Simba SC inataka kuwa au mwelekeo huo, tukio ni kubwa kwa sababu lina sura ya kiafrika au kidunia kwa hivyo maandalizi yanakwenda vizuri katika ushirikiano wa serikali, CAF, FIFA na sisi Simba SC wenyewe.”

Lakini pia Issa Masoud ameulizwa kuhusu Miquissone kuwa ataweza kufanya kama alichokifanya wakati ule na baadae kusajiliwa na Al Ahly?

“Miquissone ni sehemu ya wachezaji waliosajiliwa na Simba SC, lakini pia ni mapendekezo ya kocha kuona anafaa kumtumia kwenye mchezo huo, lakini pia anaweza kufanya kama alichokifanya wakati ule kwa sababu ni mchezaji mzuri na anaweza kufunga au kusababisha goli,” amesema mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi Simba SC, CPA Issa Masoud.

SOMA NA HII  YANGA vs CLUB AFRICAIN:...FANYEENI YOOTEE LAKINI HILI LA MWAMUZI MKILISAHAU IMEKULA KWENU....