Home Habari za michezo MO DEWJI ATEUA MABOSI WAPYA 21 SIMBA….KADUGUDA, MZEE DALALI NAO WAULA…

MO DEWJI ATEUA MABOSI WAPYA 21 SIMBA….KADUGUDA, MZEE DALALI NAO WAULA…

Habari za Simba SC

Katika kipindi cha miaka mitano iliyopita tangu tuanze safari ya Mabadililko Klabu yetu imepiga hatua kubwa sana katika nyanja mbali mbali.

Pamoja na maendeleo ambayo Klabu yetu imepiga katika kipindi hiki cha miaka mitano lakini malengo yetu bado hatujayafikia.

Mojawapo ya majukumu yangu kama Raisi wa heshima wa Simba ni kuhakikisha Uongozi na Utawala bora unazidi kuboreshwa kila wakati ili kuzidi kusukuma gurudumu la maendeleo ya Klabu yetu.

Hivyo basi baada ya kushauriana na Mwenyekiti wa Bodi na Mwenyekiti wa Klabu ya Simba, nimewateua wafuatao kuwa Wajumbe wa Baraza la Ushauri ( Advisory Board) la Klabu ya Simba.

1. Jaji Thomas Mihayo M/kiti
2. Hassan Dalali-Mjumbe
3. Ismail Aden Rage-Mjumbe
4. Evans Aveva-Mjumbe
5. Faroukh Baghoza
6. Swedi Nkwabi-Mjumbe
7. Azim Dewji-Mjumbe
8. Kassim Dewji-Mjumbe
9. Musleh Al-Ruweh-Mjumbe
10. Mohamed Nassor-Mjumbe
11. Mulamu Ng’ambi-Mjumbe
12. Octavian Mshiu-Mjumbe
13. Prof Janabi-Mjumbe
14. Hassan Kipusi-Mjumbe
15. Geofrey Nyange-Mjumbe
16. Gerald Yambi-Mjumbe
17. Moses Kaluwa-Mjumbe
18.Crescentius Magori-Mjumbe
19. Juma Pinto- Mjumbe
20. Mwina Kaduguda-Mjumbe
21. Idd Kajuna-Mjumbe

Sekretariat ya Simba itaratibu mikutano ya Baraza hili la Ushauri.

Kazi kubwa ya Baraza hili itakuwa ni kuishauri Bodi juu ya maendeleo ya Klabu yetu ya Simba, Uongozi na Utawala bora.
Asanteni
MO

SOMA NA HII  MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA SPOTI XTRA JUMAPILI