Home Habari za michezo UNAAMBIWA YANGA KAMA IMEFUATA NJIA ZA AL HILAL

UNAAMBIWA YANGA KAMA IMEFUATA NJIA ZA AL HILAL

Jambo muhimu la kujifunza ni kwamba kama timu imeweka mifumo mizuri kwenye Uendeshaji wa Klabu hata iondokewe na wachezaji wake muhimu bado itakuwa imara. Muhimu ni uendeshaji mzuri! Mifumo stahiki na viongozi imara.

Asec Mimosas licha kuondokewa na wachezaji wao muhimu lakini bado haoinyeshi kutetereka! Yani wametoa mtu Wanaingiza Mtu! Watu walihisi Asec imebomolewa baada ya Wachezaji wake muhimu kuondoka kama;

Pacome zouzoua

Aubuni Kramo

Yao Kouassi Attohoula

Mohamed Zoungrana

Hawa wote walikuwa Wachezaji Muhimu kwenye Kikosi cha Asec Mimosas, lakini Wametoa watu wameingiza watu Kazi inawndelea! Sawa kwa Al Hilal, ukiachana kuondokewa na wachezaji wake muhimu kama;

Fabric Ngoma

Makabi Lilepo

Ibrahim Imoro

Lamini Jarjou

Timu bado imeonyesha kile kile ambacho wengi hawakutarajia! Wengi hawakuamini! Ukiachana na vita Ligi kusimama Lakini watinga hatua ya Makundi Ya Klabu bingwa Afrika pongezi kwao.

Kwanini Nasema Asec Mimosas na Al Hilal ni kama Yanga SC? Yanga baada ya kuondokewa na wachezaji wao pamoja na watu wa benchi la ufundi wengi waliamini Yanga inaweza kutetereka!

Fiston Mayele Mvp

Djuma Shabani

Yanick Bangala

Benard Morrison

Na bado Benchi la ufundi likavurugika Helmy Guelish (Fitness coach), Mohamedi Nasrdeen Nabi (Head Coach), Cedric Kaze (Ass. Coach)! Nani aliamini Yanga itarudi kwenye ubora wake ule ule?

Ila uongozi Imara, mipango dhabiti, viongozi wanaoelewa Football iko vipi! Ndio wamefanya mpaka sasa ionekane Yanga ya msimu uliopita ni mbovu kuliko Hii ya Sasa Kuna Namna tunahitaji viongozi wanaojielewa ili tuweze kusonga mbele. Hongera Eng. Hersi Said.

SOMA NA HII  STRAIKA MPYA YANGA ATUMA UJUMBE MZITO SIMBA,AMTAJA MAYELE AJIPA KAZI MAALUM