Home Habari za michezo AHMED ALLY:- MVUA NI ISHARA NZURI KWA SIMBA….

AHMED ALLY:- MVUA NI ISHARA NZURI KWA SIMBA….

Habari za Simba SC

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba SC, Ahmed Ally, amesema kitendo cha mvua kunyesha kuelekea kwenye mchezo wao wa dabi, ni ishara nzuri ya ushindi kwao.

Ahmed amefunguka hayo mapema hii jana Novemba Mosi, 2023 alipokuwa kwenye mkutano wa kuwatangaza wadhamini wao wapya Kampuni ya Serengeti Breweries.

“Mvua ni ishara nzuri kwa Simba. Tukiwa katika wiki hii yenye thamani kubwa ya Kariakoo Derby tumewaletea tukio lingine kubwa la kihistoria kati ya Simba na Serengeti,” alisema Ahmed Ally.

Katika hatua nyingine, Wakati ikionekana Wachezaji wa Simba wameshindwa kuingia katika Tuzo mbalimbali msimu huu huku Yanga wakitakata.

Meneja wa Habri wa Klabu ya Simba, Ahmed Ally amezungumzia suala hilo huku akidai kuwa Simba haipewi hadhi yake.

“Kuhusu swala la tuzo za wachezaji wa Simba kutopata tuzo za wachezaji bora kwenye ligi au kutoonekana kwenye tuzo za timu bora ya mwaka kule CAF ngoja nikujibu kwa hoja.”

“Sitaki kukosea heshima lakini kuna ule mwezi Wazir Junior alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa mwezi, kwenye taarifa kuliandikwa amekuwa mchezaji bora sababu amefunga magoli 2 wakati Jean Baleke alifunga magoli 3.”

“Ni maajabu kuona aliyefunga magoli 2 kwa mwezi mzima amechukua tuzo mbele ya mtu aliyefunga magoli 3, yani wa magoli 2 ni bora kuliko wa magoli 3, inashangaza kidogo.”

“Kuhusu swala la tuzo za CAF, hizo ni tuzo za msimu uliopita, nipo hapa kuzungumza kuhusu Simba ya msimu huu. Ahsante.”

SOMA NA HII  BAADA YA MUGALU KUHARIBU....SIMBA WAPATA MTAMBO WA MAGOLI SAUZI...AMEFUNGA GOLI MBILI TU MSIMU HUU..