Habari za Yanga
Habari za michezo

AZIZI KI, ROBERTINHO ‘WAUONA MWEZI’ KWA PAMOJA….

admin November 3, 2023 8:26 pm

KAMATI ya tuzo ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imemtangaza mchezaji wa timu ya Yanga, Stephane Azizi Ki kuwa mchezaji bora wa Ligi Kuu kwa mwezi Oktoba akiwashinda Maxi Nzengeli wa Yanga na Moses Phiri wa Simba.

Azizi Ki ameifungia timu yake mabao mannekatika dakika 278 za michezo mine aliyoichezea timu yake mwezi huu.

Kamati hiyo pia imemtangaza kocha wa Simba Roberto Olivieira kuwa kocha bora wa mwezi baada ya kushinda michezo yote mitatu aliyocheza mwezi Oktoba akiifunga Tanzania Prisons 1-3, Singida Big Stars mabao 1-2 na Ihefu 2-1.

Robertinho amewashinda Miguel Gamondi wa Yanga, abdulhamid Moalin wa KMC aliongia nao fainali.

Aidha kamati imemtangaza meneja uwanja wa Higland estate mkoani Mbeya Mulale Omar kuwa meneja bora wa uwanja kwa mwezi Oktoba.

GAMONDI:- SINA PRESHA NA SIMBA ….TUTACHEZA KAMA TUNAVYOCHEZAGA NA IHEFU…. LEO UFANYE MKEKA WAKO KUSOMA ODDS HIZI KISHA UJE UNISHUKURU BAADAYE…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply