Home Habari za michezo MWENYEKITI SIMBA AMKINGIA KIFUA KENNEDY JUMA

MWENYEKITI SIMBA AMKINGIA KIFUA KENNEDY JUMA

Habari za Simba

Baada ya matokeo ya Simba kuwapa presha mashabiki, mwenyekiti wa zamani wa klabu hiyo, Ismail Aden Rage amewashauri viongozi wenzake kutulia na kutokufanya mambo kwa papara na kama kuna watu walihujumu wathibitishe na wachukuliwe hatua, huku akitaka beki Kennedy Juma aaminiwe.

Simba iliyokubali kichapo cha mabao 5-1 na kuwavuruga viongozi na mashabiki wa timu hiyo kwani ni kipigo kikubwa kwao kwa miaka ya hivi karibuni kwenye Ligi Kuu Bara.

Rage aliliambia Mwanaspoti mara ya mwisho Simba kufungwa na Yanga mabao mengi ni mwaka 1968 (5-0), wakati huo ikiitwa Sunderland, lakini ikiitwa Simba hiki ni kipigo cha kwanza kikali, hivyo lazima kishtue mashabiki na viongozi kwa ujumla.

Akizungumzia mchezo huo alikiri Yanga ilikuwa bora “Yanga ilitawazidi kimchezo tu na walikuwa bora, hivyo huoni mazingira ya haraka kuthibitisha kuna hujuma. Yanga kwa sasa ni wazuri kuliko Simba hilo halina ubishi, watu waliona kama utani kocha wao kwenda kuisoma Simba mara tatu.

“Simba ilikuwa taratibu sana wakati Yanga inakaba na kushambulia mara nyingi hivyo wakati uchunguzi unaendelea na lawama nyingi zikienda kwa wachezaji, makocha na viongozi wasisahau wapinzani wao sio timu ndogo na walijipanga zaidi yao kabla ya kuingia mchezoni.”

Kuhusu wachezaji wa Simba alisema; “Simba inatakiwa kuelewa Che Malone Fondoh anatakiwa acheze namba sita na sio beki wa kati kwani anasogea sana juu, lakini wapo wachezaji ambao wana uwezo wa kucheza na wamuamini Kennedy (Juma) ni beki mzuri na ameonyesha ubora akipewa nafasi.”

SOMA NA HII  JOB AMTULIZA MAZIMA CHE MALONE